USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 21 KUTAFUTA MIRADI YA UJENZI

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Peter Keating na Dominique anajadili mambo mbalimbali. Peter Keating anamwambia Dominique kwamba kuna mtu mmoja hampendi kabisa, anasema jina lake ni Howard Roark. Dominique anafikiria juu ya hilo kwa muda kidogo.

2. Ellsworth Toohey anawatembelea Peter Keating na Dominique na kumshawishi Peter Keating kwamba anapaswa kufanya bidii aweze kupata mradi wa jengo la Stoneridge la Gail Wynand.

3. Peter Keating anamwambia hana ukaribu na Gail Wynand hivyo hajui pa kuanzia. Ellsworth Toohey anamwambia inabidi amtumie mtu ambaye amekuwa akimtumia kupata miradi mingi zaidi. Peter Keating anamwambia ni Dominique, Ellsworth Toohey anamwambia basi ni huyo huyo.

4. Peter Keating anaonekana kusita kwa nini mke wake atumike kuweka ukaribu na Gail Wynand. Kwa ushawishi wa Ellsworth Toohey, Peter Keating anakubali kuruhusu Dominique atumike kujenga ushawishi kwa Gail Wynand ili aweze kupatiwa mradi wa ujenzi wa jengo la Stoneridge.

5. Peter Keating akiwa hayupo Dominique anamuuliza Ellsworth Toohey kwa nini yeye anataka alale na Gail Wynand.

6. Dominique anakutana na Gail Wynand, wanaongea kwa kirefu na kila mmoja bila kutegemea anashangaa jinsi mwenzake ana uelewa mpana wa mambo ya falsafa na saikolojia na mambo mengine mengi kwa ujumla. Gail Wynand anashangaa kujua kwamba Dominique aliwahi kufanya kazi kwenye ofisi zake za New York Banner na akafukuzwa kazi na yeye mwenyewe bila kujua.

7. Dominique anashangaa kwamba ile sanamu yake inamilikiwa na Gail Wynand. Gail Wynand anamwambia kwamba Ellsworth Toohey ndiye aliyeileta kwake. Dominique alikuwa hajui ile sanamu yake iko wapi.

8. Dominique anamwambia Gail Wynand kwamba amekuja kwake kwa ajili ya kumshawishi kumpatia Peter Keating mradi wa ujenzi wa jengo la Stoneridge na yuko tayari hata kulala naye kama hicho ndicho anachohitaji ili kutoa kazi kwa mume wake.

9. Gail Wynand anashangaa jinsi Dominique ameenda moja kwa moja kwenye lengo bila hata kuyumba. Anamuuliza Dominique mbona ameenda moja kwa moja hivyo, Dominique anamwambia hataki kumpotezea muda wala kumchosha na uongo uongo.

10. Gail Wynand anamuuliza Dominique kwamba anampenda sana mume wake mpaka kufanya hivyo. Dominique anamjibu kwamba hampendi ila anamdharau.

11. Gail Wynand anamuuliza kwa hiyo hajali kama mume wake atapata huo mradi au la, Dominique akasema hajali. Gail Wynand anamuuliza sasa kwa nini anafanya hivyo, Dominique anajibu kwamba ameamua tu kufanya hivyo na anapenda kuwa katika nafasi hiyo.

12. Gail Wynand akamwambia amevutiwa sana na namna amekuwa direct na kwamba yuko tayari kuingia kwenye orodha ya mahawara wake. Dominique anamwambia ni kama yeye tu anajaribu kuipa dunia kile inachotaka.

13. Gail Wynand anamwambia Dominique angependa kukutana na Peter Keating mume wake, hivyo wapange kukutana naye kesho yake kwa chakula cha jioni.

14. Wanakutana Dominique, Gail Wynand na Peter Keating kwa chakula cha jioni. Peter Keating anaonekana kufurahia sana kupata chakula cha jioni katika eneo la wazi wakiwa na Gail Wynand.

15. Gail Wynand anamwambia Peter Keating kwamba ameshapata mradi huo. Peter Keating anashangaa mbona imekuwa ghafla sana kwani alitegemea huo ndio uwe mwanzo wa kufahamiana kwao kupewa mradi huo.

16. Gail Wynand anamsifia uzuri wa Dominique mbele ya Peter Keating, Peter Keating anaonekana kutofurahia mazungumzo ya namna hiyo.

17. Gail Wynand wanaondoka na Dominique kwenda safari ya mbali kwa siku kumi kwa boti ya kifahari ya Gail Wynand inayoitwa “I DO”.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *