UJENZI WA HOTELI YA KITALII.

Ujenzi wa hoteli za kitalii na hata hoteli za aina zozote ni ujenzi kama ujenzi mwingine isipokuwa huu unahitaji ubunifu mkubwa kwenye ramani na mazingira yake. Hoteli ni tofauti na nyumba za kawaida au majengo ya ofisi kwa sababu hotelini ni sehemu ya kwa ajili ya kupumzika na kustarehe hivyo hoteli inapaswa kupewa kipaumbele kikubwa kwenye ubunifu wa ambao utampa mteja hali ya kuhisi anastarehe na kufurahia ubunifu wa kimazingira na majengo sambamba na mpangilio wa vitu, nafasi na hata watu.

Hivyo kufikiria kuanza kujenga hoteli ya namna yoyote ile ni muhimu sana kuanza kufikiria ule utaalamu wa kibunifu ambao hoteli inapaswa kuwa nao kwa kumtafuta mtu mbunifu majengo na timu yake nzima kushirikishana mawazo ili kuweza kutambua namna sahihi ya kuuendelea mradi huo. Umuhimu huu unakuja kwa sababu pia hoteli tofauti na majengo mengine hauhusishi jengo peke yake bali inaanzia kuanzia ubunifu wa ndani ya jengo(interior design), mazingira ya nje ya jengo(landscape design) pamoja na jengo lenyewe. Pia mpangilio wa kila kitu ni muhimu sana katika kuongeza mvuto.

Hoteli na mazingira yake yanapokuwa yamezingatia ubunifu wa hali ya juu yanaongeza mvuto wake maradufu na ndio yanakuwa chanzo cha wateja kupenda kutembelea na kutumia hoteli hiyo mara kwa mara na hasa kuleta marafiki. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka sana kutafuta hoteli zinazovutia katika mazingira yao kwa mafanikio kidogo kwa sababu tu ya kukosekana kwa ubunifu sahihi wa hoteli na lodge mbalimbali, lakini jambo la kushangaza ni kwamba hata kwa ujenzi wa hoteli za kawaida za mitaani gharama ya kutengeneza ubunifu kupitia ramani ni kidogo sana ukilinganisha na ile thamani ambayo jengo husika linapata na faida itakayotokana na ubunifu huo. Ni muhimu sana ili kujenga thamani sahihi kabla ya kuanza kujenga hoteli kuzingatia sana ubunifu wa kitaalamu.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *