UJENZI WA MAJENGO YA SHULE.

Ujenzi wa majengo ya shule ni ujenzi kama ujenzi mwingine wowote ule isipokuwa mpangilio wa kisanifu kwa majengo ya shule ndipo utofauti unapotoka. Changamoto ni kwamba baadhi ya watu kwa kutokujua madhara yake huamua kujenga shule kwa maamuzi yao binafsi bila kuhusisha wataalamu wa usanifu na uhandisi kitu ambacho hupelekea mazingira ya shule kukosa mpangilio sahihi na unaoendana na mazingira ya shule.

Ujenzi wa shule unatofautiana kidogo na ujenzi wa nyumba ya kuishi kwa sababu mara nyingi shule haina urembo mwingi sana kama nyumba ya kuishi lakini shule kwa upande wake inahitaji umakini sana katika mpangilio. Shule kwa sababu ni eneo la umma au watu wengi inahitaji utaalamu mkubwa wa mpangilio wa maeneo yake na majengo yake kadiri ya uhusiana wa eneo nae neo au nafasi na nafasi kuhakikisha hakuna usumbufu mkubwa wa maingiliano baina ya maeneo yake.

Unapotaka kuanza kujenga shule kwanza unahitaji kufahamu mambo yote utakayojumuisha katika shule yako kadiri ya uhitaji wako ile uweze kuhakikisha unakuwa na mpangilio sahhi wa kila kitu tangu mwanzoni hata kama baadhi ya majengo utakuja kujenga baadaye. Unapaswa kuwa na ule mpangilio mkuu wa eneo (masterplan) iliyopangilia kila kitu mwanzoni iwe kitajengwa sasa au baadaye. Hilo litasaidia kufanya ujenzi kwa usahihi, kuepuka hasara na kuepuka majuto ya muda mrefu baada ya kuwa ujenzi umashafanyika kimakosa na nafasi ya kubomoa kabisa haipo kwani ni hasara isiyobebeka.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *