UJENZI WA KIWANDA.

Ujenzi wa kiwanda sio ujenzi mgumu kama wengi wanavyoweza kufikiria bali jambo muhimu ni kupatikana kwa taarifa sahihi kuhusu kiwanda husika kuanzia uhusiano kati ya nafasi na nafasi, madhara ya kiafya na kimazingira ya mashine ndani ya kiwanda n.k., Wakati mwingine ujenzi wa kiwanda jambo utazingatia mzunguko mzima wa shughuli za ndani ya kiwanja lakini kazi ya kuchora ramani ya kiwanda inaweza kufanywa kwa mfumo wa ghala kubwa kisha baadaye mashine za kiwanda kuja kuwekwa kwa namna ambayo inaendana na shughuli hizo. Hata hivyo ni lazima michoro ya kiwanda iwe imefanyika kuendana na mpangilio wa kila kitu na shughuli zote.

Ujenzi wa kiwanda ni ujenzi kama ujenzi mwingine wowote isipokuwa ramani ya kiwanda ndio huja na vipaumbele tofauti vinavyoendana na kiwanda husika. Mara nyingi na mara zote ramani ya kiwanda huzingatia sana michakato ya shughuli za ndani za kiwanda ngazi kwa ngazi kuanzia pale ambapo malighafi zinaingia kiwanda mpaka pale bidhaa zinapotoka kiwandani. Mchakato wa shughuli hizi huhitaji umakini mkubwa kwenye kuzipangilia kutokana na madhara makubwa ya kiafya, kimazingira na hata usalama na ubora wa bidhaa zenyewe ambao ndio huamua nguvu yake sokoni.

Hivyo ni muhimu sana kabla ya mtu kuanza kujenga kiwanda kufikiria kwanza mchakato mzima wa shughuli za kiwandani utakavyoenda kisha kumwita mtaalamu wa kuchora ramani ya kiwanda na kushirikiana naye mawazo juu ya ujenzi wa kiwanda husika. Ikiwa kuna timu inayohusika na uzalishaji wa bidhaa zinazotegemewa kuzalishwa katika kiwanda husika ni vyema sana pia wakahusika katika kuchangia mawazo wakati wa mkutano na mtaalamu au wataalamu wa kuchora ramani ya kiwanda hicho. Baada ya hapo zoezi linalopaswa kufuatia ni uchoraji wa kitaalamu wa kiwanda husika ukiwa umezingatia sana yote yaliyojadiliwa katika kikao sambamba na uzoefu wa msanifu majengo na mhandisi wa kiwanda husika kwa pamoja kuja na michoro.

Mwisho itapatikana michoro sahihi sana ambayo ndio itakuwa imebeba maelekezo yote ya namna ujenzi huo unavyopaswa kufanyika na hata vifaa na malighafi zinazokwenda kutumika. Kwa kuzingatia haya utaweza kuwa na kiwanda kinachofanya kazi kwa usahihi sana kikiwa pia na mwonekano bora na unaovutia ambao unakiongezea hadhi kubwa zaidi kwa namna kimepangiliwa kitaalamu.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *