UJENZI WA KANISA.

Watu wengi wamekuwa wakiulizia sana kuhusu ujenzi wa jengo la kanisa, utaalamu wake na gharama zake. Baadhi wamekuwa wakiwa na fikra na mitazamo tofauti juu ya ujenzi huu huku wengine wakiwa hawana uelewa mchakato wake ulivyo. Kiuhalisia ujenzi wa kanisa ni ujenzi kama ujenzi mwingine isipokuwa utofauti kati ya kanisa moja na jingine unategemea na mahitaji ya kanisa husika sambamba na shauku na mategemeo ya waumini wa kanisa hilo.

Hata hivyo mara nyingi muonekano wa kanisa ndio hutambulisha thamani yake na hilo pia huchangia sana kuvutia waumini katika kanisa hilo kwa kile wanachokiona kwa muonekano wa nje sambamba na mambo mengine. Hivyo kabla ya kufikiria ujenzi wa kanisa ni muhimu kutafakari kwanza ni kanisa la aina gani linalohitajika kisha kuwashirikisha waumini na kisha kwa pamoja kujadili pamoja na wataalamu wa usanifu majengo na uhandisi kujua yale haswa yanayohitajika.

Kushirikisha waumini na wadau mbalimbali kutasaidia kuhamasisha na kufanikisha harambee za michango ya ujenzi kwa sababu ndio watakaokuwa wamechangia mawazo ya ujenzi wakiwa wanajua bajeti sahihi na kile ambacho kipo ndani ya uwezo wao na kwa muda ambao wanao katika hilo. Kwa ushirikiano na timu ya wataalamu ni rahisi kuweka mipango sahihi katika kuliendea hilo.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *