UTAJISIKIAJE KAMA UTAJENGA NYUMBA AMBAYO NI MFANO WA KUIGWA?

Mtazamo wa mtu ni kitu chenye nguvu sana, hicho ndicho huathiri taswira yake nzima kwenye maisha, mtazamo ndio ambao hupelekea namna maisha ya mtu yanavyokuwa katika uhalisia. Hili suala la mtazamo limebadilisha maisha ya watu wengi kuelekea kule ambako wamekuwa wakifikiri zaidi na kuwa kile ambacho kimekuwa kikitawala mitazamo yao. Wanafalsafa wote duniani na dini mbalimbali wamekuwa wakiamini katika hiki kitu kimoja kwamba mtu anakuwa kile ambacho kimetawala fikra zake.

Sasa tunapokuja kwenye suala la ujenzi wa nyumba yako ambayo umekuwa ukiifikiria kwa miaka mingi zaidi suala la mtazamo linaingia sana hapa. Kama umekuwa unafikiria kuwa na nyumba ilimradi una nyumba basi hilo ndilo litakalotokea, lakini kama umekuwa ukifikiria kuwa na nyumba fulani yenye upekee wa aina yake basi kwa hakika hilo ndilo linalokwenda kutokea pia. Sasa ikiwa tu unahitaji kujenga nyumba ambayo itakuwa ni ya kipekee na ya mfano kwa uzuri na mpangilio wake basi unapaswa kuanza kuimarisha mtazamo huo ndani ya akili yako na kuanza kuchukua hata sasa hivi.

Hata ya kwanza ya kufanikisha lengo lako hilo ni kuonana na mtaalamu wa usanifu majengo na kujadiliana naye juu ya mtazamo wako na mategemeo yako hayo kisha kupanga kwa pamoja namna sahihi ya kulifikia hilo. Ukweli ni kwamba kufanikisha ndoto yako hiyo itakupa furaha na amani ya ndani ya moyo ambayo itaendelea kurudi kila unapotazama kile ambacho ulipanga na kukifanikisha. Hebu pata picha hivi utajisikiaje pale ambapo watu wanakusifu na kukupongeza kwa ubunifu na akili kubwa uliyonayo kuweza kufanikisha kujenga nyumba bora sana na ya mfano?

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *