KUHUSU UJENZI HUPASWI KUKATA TAMAA.

Watu wengi wanapokuwa vijana wadogo wanaokua huwa na ndoto kubwa sana kwenye maisha yao za kufanikisha mambo mengi sana makubwa. Lakini kwa bahati mbaya wengi ndoto zao huendelea kufifia kadiri ziko zinavyoendelea Kwenda mbele, japo baadhi hujitahidi kupambana nazo kwa nguvu lakini bado kuna kundi kubwa ambalo huishia kukata tamaa kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele. Kwa sehemu kubwa kukata tamaa hutokana na mtu kuzungukwa na jamii ya watu ambao wana mtazamo hasi sana kwenye maisha yao na hasa jamii ambazo hazina watu wengi waliofanya mambo makubwa kwenye maisha au ambao hawajifunza na kuamini kwa watu waliofanya mambo makubwa kwenye maisha iwe ni ndani ya jamii yao au maeneo mengine duniani.

Ndoto hizi kubwa ambazo watu wengi huwa nazo ni katika nyanja nyingi mbalimbali katika maisha ikiwa ni pamoja na nyumba za maisha yao. Watu wengi huwa na ndoto kubwa za kuja kuishi kwenye nyumba kubwa na za kifahari sana katika maisha yao wakiwa kwenye umri wa ujana lakini kwa wengi ndoto huendelea kuyeyuka pale wanapokutana na uhalisia wa maisha na taratibu huanza kuamini kwamba ndoto zao hizo haziwezekani kufanikiwa na mwisho kuamua kuachana nazo. Japo wengine huja kuona kwamba ndoto zao zilisababishwa na utoto zaidi na kwamba hakuna umuhimu mkubwa kuendelea kung’ang’ania kuzifikia lakini ukweli ni kwamba hilo linachangiwa pia na wao kuzikatia tamaa.

Lakini kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba ndoto ambazo hufanikiwa kutokana na kukua kwa kipato huchelewa kwa sababu mafanikio ya kifedha nayo yanachelewa pia. Ikiwa mtu ataweka bidii kubwa kabisa katika maisha yake ni wazi kwamba lazima atafikia ndoto zake hizo lakini muda atakozifikia utategemea na namna bidii yake na njia anazotumia kuzifikia. Hata hivyo kwa uzoefu wangu binafsi nimekuja kugundua kwamba uwezo wa watu wengi wanaofikia kuishi kwenye nyumba za ndoto zao huja kuanzia katika angalau umri wa miaka 50 na kuendelea. Kabla ya umri huo ni watu wachache sana huweza kufikia ndoto zao na zaidi ni wale ambao taaluma zao au fani zao huwaletea mafanikio makubwa katika umri mdogo kama vile wachezaji wakubwa, wasanii wakubwa n.k.,

Hivyo kwa mtu ambaye una ndoto za kuishi katika nyumba ya kifahari sana ya ndoto zako, badala ya kukata tamaa kati umri wa miaka ya 20 na 30 ni vyema ukaongeza bidi kubwa katika mapambano yako na usikubali kabisa kukatia tamaa ndoto yako hiyo. Endelea kuweka bidii fokasi kuelekea kwenye ndoto zako na kuhakikisha unaelekea kwenye kuishi ndoto yako ambayo utajivunia sana katika maisha yako iwe kama urithi kwa vizazi vinavyofuata nyuma yako kuiga na kukuenzi kwayo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *