GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA.

Wote tunafahamu kwamba ujenzi wa nyumba ni jambo linalohusisha gharama kubwa, na kwa watu wengi ndio mradi wa gharama kubwa kuliko kitu kingine chochote katika maisha. Sababu hii imepelekea kwamba watu wengi kuogopa sana gharama za ujenzi kiasi kwamba mara zote wamekuwa wakifikiri namna ya kupata ujenzi wa bei nafuu. Hata hivyo kwa kupitia njia ya kujenga kwa awamu ndogo ndogo, changamoto ya gharama imepungua kuwa mzigo mkubwa kwa wengi badala yake inahitajika zaidi nidhamu katika matumizi ya fedha.

Lakini pamoja na yote haya watu wanakosea sehemu moja. Watu wanafikiri kuna njia za kimiujiza za namna ya kupunguza gharama za ujenzi hasa kupitia aidha vifaa vya tofauti sana au namna ya kitaalamu. Watu wengi wanaojenga ambao hawakuwahi kujenga kabisa hapo kabla wanakuja kugundua kwamba gharama za ujenzi ni kweli ziko juu kuliko walivyokuwa wanafikiria na hakuna namna ya kuzipunguza kwa kiasi kikubwa sana bila kuathiri ubora au matumizi ya jengo lenyewe. Uhalisia huu huwa unawashangaza watu lakini wanajikuta hawana namna nyingine zaidi ya kukabiliana nayo.

Ipi sasa ni njia sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi? Njia sahihi za kupunguza gharama za ujenzi ni kupunguza ukubwa wa jengo. Japo ni kweli kwamba mtu unaweza kuwa na njia nyingine za kupunguza gharama za ujenzi kupitia aina ya vifaa unavyochagua na ufundi unaochagua katika mradi wako lakini hayo hayaleti unafuu mkubwa. Unafuu mkubwa wa gharama unakuja na kupunguza ukubwa wa jengo kadiri ya utakavyoona inakufaa, na kwa kuwa ukubwa wa gharama unategemea na uwezo wa mtu basi utapunguza gharama kadiri ya wewe mwenyewe unavyoona ni nafuu kwako.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *