UNAWEZA KUFANYIWA RAMANI NYINGINE YA UJENZI NZURI ZAIDI YA HIYO.

Watu wengi wamekuwa wanapata changamoto kwenye kuelewa kitu kimoja katika ujenzi kwamba picha au ramani uliyoiona haikutengenezwa kwa ajili yako na hivyo sio rahisi ikufae na kwamba utaweza kupata manufaa mengi utakapofanyiwa kazi mpya inayoendana na mawazo tuliyonayo. Kuna watu pia hufikiri kwamba ramani nyumba wanayoiona inaweza kufanyiwa kazi ikibaki hivyo hivyo na ikajengwa bila kufanyiwa mabadiliko yoyote ya tofauti sana.

Hili limekuwa likisababisha hata mtu kufikiria kwamba tofauti na hiyo anayoiona basi atatakiwa kutafuta sehemu nyingine. Ukweli kwamba hakuna kazi uliyoiona popote duniani ambayo hatuwezi kuifanya tena kwa viwango vya juu kuliko hiyo uliyoiona. Tuna uwezo wa kufanya kazi yoyote kwa namna yoyote na ikawa bora zaidi na inayoendana na wewe kwa usahihi kabisa. Pia kupitia majadiliano ya baada ya kila hatua tunaweza kufanikisha mpangilio wa namna yoyote ndani au nje ya jengo husika.

Hivyo ikiwa mtu unahitaji kitu chochote katika ujenzi au katika ramani ya ujenzi hupaswi kuwa wasiwasi au kuwaza kama kitaweza kufanyika kwa ubora kama unaotaka au kufikiria, unachotakiwa kufahamu kwamba kuna nafasi kubwa zaidi kwamba kitafanyika kwa ubora zaidi huo unaouona.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *