USIOGOPE KUANZA UJENZI, ANZA NA RAMANI.

Kuna watu wengi sana hasa vijana hutamani sana kujenga lakini wanapoulizia gharama za ujenzi na kuambiwa hukata tamaa na kuamua kuahirisha kabisa kujenga. Ukweli ni kwamba gharama za ujenzi ni kubwa ukilinganisha na kipato cha watu walio wengi wa kipato cha kati. Hivyo mtu anapoangalia kipato chake kwa mwezi akilinganisha na gharama za ujenzi hukata tamaa kabisa na kuona kwamba suala la kujenga haliko ndani ya uwezo wake. Hata hivyo licha ya kwamba gharama za ujenzi ni kubwa lakini bado kuna watu wa vipato hivyo hivyo wamekamilisha ujenzi wa nyumba zao na wanafurahia maisha ndani ya nyumba zao wenyewe.

Je tembo analiwa vipi? Ukitaka kumla tembo ukamwangalia tembo mzima alivyo utakata tamaa lakini ukweli ni kwamba unaweza kumla tembo na kummaliza kabisa peke yako. Na ukitaka kumla tembo utaanza kwa kumkata vipande vidogo vidogo na kula mpaka kumaliza. Hivyo ukitaka kujenga nyumba ambayo ni gharama kubwa utaanza kwa awamu na kwenda hatua ndogo ndogo mpaka kumaliza nyumba. Lakini hata hivyo hatua ya kwanza baada ya kupata kiwanja ni unaanza na ramani. Jambo muhimu la kuhakikisha ni kwamba unatengeneza ramani bora sana nay a kisasa ili kwanza ikupe motisha na shauku ya kuweka bidii katika kuijenga na pili ni iwe nguvu zako unazipeleka kwenye kitu chenye ubora na kinachostahili kuhangaikiwa.

Ramani itakupa mwongozo mzuri na sahihi w akule ulikoamua kwenda na pia itakusaidia kuweza kutengeneza mahesabu ya gharama ambayo ndio yatakuwa mwongozo wa bajeti yako katika kila awamu. Baada ya hapo nasi utaanza na hatua za awali taratibu na kuendelea hatua kwa hatua huku ukiwa unapumzika mpaka pale utakapokamilisha jengo lako. Faida za kuamua kuanza ni kwamba kuna pesa nyingine unazipata na kuamua kuzifanyia mambo ambayo sio muhimu sana lakini ikiwa unafahamu kwamba una ujenzi itakuwa kila ukipata hela unapeleka kwenye ujenzi na baada ya mua utashaangaa umepiga hatua kubwa ambayo hukutegemea kabisa ungeweza kupiga kwa kipindi hicho. Chukua hatua sasa anza mara moja.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *