KWA NINI WATU WENGI WANAKOSEA KWENYE MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI.

Moja kati ya udhaifu mkubwa tulionao binadamu ni huwa tuna kawaida ya kulinganisha vitu kwa muonekano wa nje. Lakini bado ingekuwa afadhali kama tungekuwa tunafananisha vitu kwa muonekano wa nje lakini kwa kuchunguza kwa makini na kwa undani kama kweli vitu hivyo vinalingana kwa uhalisia hata kwa huo muonekano wa nje. Vitu vingi ambavyo kwa muonekano wan je ukivifuatilia kwa karibu zaidi utagundua havifanani wala kulingana pia achilia mbali kuvipima kabisa lakini sisi kwa mtazamo wa nje huwa tunachukulia kwamba vitu hivyo vinalingana.

Tukija kwenye ujenzi hali haiku tofauti sana, watu wengi hutazama miradi au majengo au nyumba mbalimbali na kujaribu kuzilinganisha bei na nyingine kuona kama watakuwa wametumia gharama sahihi au wamefanyiwa udanganyifu. Na mara nyingi karibu mara zote hukuta bei ni tofauti licha ya kudhani kwamba miradi hiyo inalingana. Ukweli ni kwamba licha ya kwamba miradi mingi au nyumba nyingi ni vigumu sana kulingana ukubwa kamili lakini hata kama zitalingana kila kitu yaani kutumika kwa ramani hiyo hiyo kwenda kujenga mradi mwingine wa mtu mwingine bado gharama zitatofautiana kutokana na sababu nyingi sana mbalimbali.

Sababu za miradi kutofautiana bei japo kuwa kweli ikiwa ramani ni hiyo hiyo maeneo mengi kama vile vifaa yatakuwa sawa lakini bado bei za vifaa zitatofautiana kulingana na ubora na upekee na bei za ufundi pia zitatofautiana kwa sababu hiyo hiyo. Sababu ambazo hupelekea bei kutofautiana kati ya mradi mmoja na mwingine nyingi sana kiasi kwamba haipaswi kuwa jambo la kushangaza zaidi kinachopaswa ni sababu yenyewe kujulikana na kuwekwa wazi ili kusaidia katika kuboresha huduma za ujenzi na kuongeza thamani kwenye fani ya ujenzi kwa ujumla.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *