UTAALAMU WA KUCHORA NA KUJENGA NYUMBA YOYOTE NDIO UNAOTUMIKA KWENYE KUCHORA NA KUJENGA NYUMBA/JENGO LINGINE LOLOTE.

Mara kwa mara nimekuwa nikikutana wateja mbalimbali wenye mahitaji tofauti tofauti ya kila namna. Licha ya kwamba mahitaji haya yamekuwa yakija kwa upekee tofauti tofauti kuna kitu kimoja kimekuwa kikinishangaza na kuleta usumbufu kidogo. Jambo hilo ni wateja kuamini kwamba mtalaamu anatakiwa awe alishafanya jengo la aina fulani ili kuwaza kufanya mradi wake huo. Ingawa ukweli ni nimeshafanya miradi ya aina zote lakini mtazamo huu kwa upande wa mteja hauendani na uhalisia wa taaluma ya usanifu na uhandisi wa majengo.

Mtaalamu wa majengo katika eneo la usanifu, uhandisi na mengineyo ana uwezo wa kufanya mradi wa jengo lolote hata ikiwa hajawahi kufanya hivyo hapo kabla, ambacho kinatakiwa kufanyika ni mtaalamu huyo apewe taarifa za kutosha za eneo la ujenzi na mahitaji ya kimatumizi ya jengo husika. Ambacho mtaalamu anahitaji ni kufahamu namna jengo litakavyokuwa linatumiwa na kiasi cha mizunguko ndani ya jengo na moja kwa moja atafanya kazi nzuri na sahihi. Lakini hata ikiwa kwamba anahitaji uzoefu wa mradi husika bado kuna majengo mengi sana katika mazingira yake na hata mitandaoni ambapo anaweza kufanya utafiti na kupata ile taarifa anayohitaji ili kutatua changamoto fulani ya kisanifu au kihandisi katika jengo husika.

Hivyo suala la wateja kutaka kwanza mtaalamu awaonyeshe kazi aliyofanya katika mradi husika kwa mfano kiwanda, shule, hospitali, msikiti, kanisa, uwanja, karakana, nyumba ya kuishi sio uhalisia kwa sababu kitaaluma hivyo vyote ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wake kwani kanuni anazotumia ni zile zile anazotumia katika ujenzi mwingine wowote. Hivyo mteja anapaswa kuondoa shaka kabisa, na anachopaswa mteja ni kujua hasa kile anachokitaka kwa usahihi na kukielezea kieleweke vizuri kwa mtaalamu wa kufanya ujenzi na atapatiwa anachotaka, na hata ikiwa kuna mabadiliko kidogo bado kazi itafanyiwa yale marekebisho husika mpaka amefanikisha kile hasa anachokitaka.

Hivyo mteja hapaswi kuwa na wasiwasi wowote juu ya kile anachokwenda kufanyiwa kwani kanuni zinazotumika ni zile zile na mwisho wa siku matokeo yataendana na kile haswa alichodhamiria.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *