UIMARA NA USAHIHI WA MIFUMO YA HUDUMA NDANI YA JENGO.

Kabla hatujaingia kujadili mada ya leo kwanza tufahamu ni nini maana ya mifumo ya huduma ndani ya jengo. Mifumo ya huduma ndani ya jengo ni ile mifumo yote inayotoa huduma endelevu ndani ya jengo wakati jengo likitumika. Yaani ujenzi wa jengo ukishakamilika kuna huduma nyingine huwa ni endelevu ndani ya jengo kama vile mifumo ya maji, umeme, mifumo ya baridi na joto ndani ya jengo, mifumo ya lifti za kupanda na kushuka na ngazi zinazotembea n.k., Mifumo hii ya huduma ndani ya jengo hufanywa mhandisi mtaalamu wa huduma au mhandisi huduma maarufu zaidi kama “service engineer”.

Tofauti na mifumo mingine kama vile mifumo ya uhandisi, mihimili, mifumo ya uwazi, mifumo yap aa, sakafu n.k., mifumo ya huduma ndani ya jengo huwa ni endelevu wakati wa matumizi ya jengo tofauti na hiyo mifumo mingine ambayo ni mfu kwani ujenzi ukamalizika nayo haiendelei kuwa kwenye mizunguko au kusukumwa na nishati ili kufanya kazi. Mifumo ya huduma huendelea kuwa katika mizunguko wakati wote na mara nyingi huhitaji ukarabati wa mara kwa mara.

Sasa tofauti na mifumo mingine ndani ya jengo ambayo haiko kwenye mizunguko ambayo hukaguliwa wakati ujenzi unaendelea, uimara na usahihi wa mifumo ya huduma ndani ya jengo hupimwa ara baada ya kumaliza kuiweka au kuifunga mifumo hiyo. Mifumo ya huduma tunasema inawekwa au kufungwa kwa kiingereza “installation” badala ya kujenga kwa sababu huo ndio uhalisia wake na ni rahisi kubadilisha au kufanya ukarabati kuliko mifumo mingine. Kwa hiyo sasa uimara wa mifumo ya huduma ndani ya jengo kama vile umeme, lifti, mifumo ya maji safi na maji taka, mifumo ya baridi na joto ndani ya jengo, mifumo ya ngazi zinazotembea hupimwa uimara wake kwa kuijaribu baada ya kuifunga.

Baada ya ujenzi kukamilika au angalau baada ya kazi ya kuweka mifumo ya huduma kukamilika kinachofuata ni kupima uimara wa mifumo hiyo kwa kuiwasha au kuiwekea nishati yake kama vile maji kwenye mabomba na umeme kwenye mifumo ya umeme kuona kama itafanya kazi kwa usahihi au itaonyesha maeneo yenye hitilafu. Ikiwa majaribio hayajaonyesha kasoro zozote au hitilafu za kimifumo basi tunaweza kusema mifumo husika ya huduma iko imara na sahihi kabisa. Lakini ikiwa mifumo hiyo itaonyesha hitilafu kwenye mifumo ya umeme kama vile shoti au kutokufanya kazi au mifumo ya maji kuonyesha kuvuja ni kwamba mfumo husika au imara. Hii ndio njia sahihi ya kupima uimara wa mifumo na usahihi wa ufundi wa mifumo husika ndani ya jengo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi

Whtasapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *