ENEO LA UJENZI HALITAKIWI KURUHUSIWA MTU ASIYEHUSIKA KUINGIA.

Mamlaka na taasisi zinahusika na mambo mbalimbali usalama katika maeneo ya kazi zimeainisha mazingira na taratibu mbalimbali za kazi katika maeneo husika. Taratibu hizi licha ya kwamba huwa hazifuatwa kwa uhakika na wakati mwingine zinapuuzwa sana lakini zimewekwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali na yote yakiwa na lengo na umihumu fulani. Moja kati ya taratibu zinazojulikana kwenye maeneo ya ujenzi ni pamoja na kuzungushia uzio(hoarding) kwenye eneo lolote ambalo mradi wa ujenzi unafanyika. Kuweka uzio umekuwa ni utaratibu unaofahamika lakini ambao pia umekuwa ukisisitizwa na mamlaka zote ikiwema mamlaka zinazosimamia usalama mahali pa kazi.

Lengo la kuweka uzio katika eneo la ujenzi linajumuisha kuhakikisha eneo la ujenzi liko salama lakini pia kwa kuwa eneo la ujenzi lina hatari nyingi kiafya na hata hatari ya kupoteza maisha basi linazuiwa ili kumkinga mtu asiyehusika na ambao hajavaa mavazi sahihi ya usalama kuumia au kupata majanga makubwa zaidi kutokana na shughuli zinazoendelea kwenye eneo la ujenzi. Jambo lingine muhimu linalozingatia katika kuweka uzio na kuzuia watu wasiohusika kuingia kwenye eneo la ujenzi ni pamoja na usalama wa vifaa vya ujenzi kutoka kwenye hatari ya kuibiwa au kuharibiwa na watu wa nje walioingia kwa nia isiyo sahihi.

Hivyo eneo lolote ambapo ujenzi unaendelea hata kama litakuwa bado halijazungushiwa uzio kwa sababu zozote zile linatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na marufuku ya mtu yeyote asiyehusika kuingia katika eneo hilo. Kuzuia watu wasiohusika kuingia katika eneo la ujenzi kutasaidia pia kurahisisha kudhibiti wale wahusika wa ndani dhidi ya kujilinda na hatari zote zilizopo katika eneo la ujenzi sambamba na kudhibiti wizi na upotevu wa vifaa vyote vilivyopo au vinavyotumika eneo la ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *