KUNA NAMNA NYINGI ZA KUIBORESHA NA KUIREKEBISHA NYUMBA YAKO YA SASA KUWA YA KISASA ZAIDI.

Maboresho na ukarabati ni kati ya vitu ambavyo ni muhimu sana katika nyumba ambayo imeshatumika kwa miaka kuanzia mitano na kuendelea kwa sababu mambo mengi yanaenda yakibadilika kila siku na hivyo vifaa na teknolojia inabadilika pia hivyo kufanya mabadiliko ni jambo muhimu la kufikiria na kuzingatia. Lakini pamoja na hayo mara nyingi wakati tunajenga nyumba unakuta tuko katika hali fulani ya maisha kiuchumi na hata kimtazamo na kadiri siku zinavyokwenda hali za maisha zinabadilika kuanzia kiuchumi, kimitazamo na hata ukomavu wa kiakili na kifikra, malengo na matamanio hivyo mtu utakuta hata machaguo yake aliyokuwa nayo miaka mitano au kumi iliyopita kwa sasa yamebadilika kabisa.

Tunaweza kuchukulia mfano makampuni ya simu za mkononi, computer na magari, unaweza kuona kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita mambo yameshabadilika kwa ukubwa kiasi gani. Fikiria simu ambayo ulikuwa unaitumia miaka kumi iliyopita ukapewa leo hii itakufaa kiasi gani, unaona wazi kwamba ukiletea leo unaweza hata kuitupa jinsi itakavyokuwa iko nyuma ya wakati na haikidhi tena mahitaji yako ya leo. Sasa tukirudi kwenye nyumba napo kasi ya mabadiliko katika zama hizi ni kubwa sana pia, ukiangalia nyumba nyingi zilizojengwa miaka kumi mpaka kumi na tano iliyopita ukizilinganisha na nyumba za kisasa zinazojengwa kwa sasa hivi kuna mabadiliko makubwa kuanzia ya mvuto wa kimuonekano mpaka matumizi ya ndani ya jengo.

Changamoto iliyopo ni kwamba baadhi ya watu kwa upande wa nyumba hawana mtazamo chanya na wa wazi juu ya mabadiliko, wao wana mtazamo kwamba ukishajenga nyumba leo hii basi ndio umemaliza na utakachofanya baada yah apo labda ni usafi tu. Hata hivyo baada ya miaka kadhaa kupita watu huoni kweli kuna mabadiliko mengi katika mazingira yao ya nyumba nzuri kila mahali na zilizokamilika zaidi kimahitaji tofauti na ya kwao ambayo ni kama inaonekana ni ya nyakati za nyuma kidogo na kufikiri kwamba wanaweza kubaki tu hivyo hivyo. Habari njema ni kwamba nyumba yoyote ambayo imejengwa, hata kama ilijengwa kizamani kiasi gani bado ina nafasi ya kuboreshwa na kuwa na kila kitu cha kisasa mpaka muonekano kuzidi nyumba zote katika mji husika.

Kwenye suala la gharama kutakuwa na gharama za kurudia kuchukua taarifa yote na vipimo vya kila kitu kwenye nyumba ya sasa na kisha kwenda kufanya upya ramani ya kisasa kwa kufanya mabadiliko makubwa ya mipangilio ya vyumba ndani ya jengo au hata kuongeza vyumba na hata muonekano wa nje wa kisasa wa jengo. Kisha ukarabati na maboresho ya jengo hilo kufuatia kadiri ya ramani ya ukarabati na maboresho ilivyofanyika bila kuachana na kila kitu wala kuhamisha jengo kwenda sehemu nyingine. Kwa namna hii unapata kile unachokitamani bila kuhama ulipo au kuanza mradi mpya eneo jingine.

Lakini pia wakati mwingine inawezekana nyumba yako ilijengwa vibaya kwa namna ambayo haikuvutii kabisa na ungependa ifanyiwa mabadiliko na maboresho kuendana na matamanio yako basi hilo pia linaweza kufanyika na ukapata hasa kile unachokitaka. Hili linajumuisha pamoja na mbadala wa kubadili jengo kutoka kuwa nyumba ya kawaida isiyo ya ghorofa kuelekea kwenye nyumba ya ghorofa au nyumba ya ghorofa moja kuelekea kuwa ya ghorofa mbili au tatu na kuendelea. Mabadiliko haya watu wengi wamekuwa wakifikiria labda ni mabadiliko magumu au yasiyofaa lakini ukweli ni kwamba kwa kutumia utaalamu wa taaluma ya usanifu majengo na uhandisi ni mabadiliko yanayoweza kufanyika kwa usahihi na umakini kuliko hata ilivyofanyika mwanzoni.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *