KAZI YA UBUNIFU YA USANIFU WA MAJENGO INAFANYIKA KWA VITENDO.

Mahitaji ya wateja katika miradi ya usanifu au ubunifu majengo yamekuwa yakipatikana kupitia majadiliano katika mteja au wateja na washauri wa kitaalamu katika ubunifu majengo wakati mwingine sambamba na uhandisi majengo. Hilo ni jambo sahihi kabisa kwa sababu hiyo ndio namna pekee ambapo mteja anaweza kupata kile hasa ambacho anakitazamia na kukitegemea kwa kuwa kwa kusikilizwa anaeleza kwa maneno na hata vitendo mahitaji yako hayo.

Hata hivyo kwa bahati mbaya aidha kwa kujua au kutokujua watu wamekuwa wakijadili kazi ya usanifu kwa kutaka kukamilisha kila kitu hapo hapo kwenye majadiliano na kubakisha utekelezaji pekee. Lakini hiyo sio namna sahihi ya kufanya kazi ya usanifu kwa sababu kazi ya usanifu inafanyika kwa vitendo na ubunifu wakati huo mtu akiendelea kuifikiria kwa kina wakati anaifanya na hapo ndipo anakuwa anatatua changamoto nyingi sana wakati wa mchakato huo.

Kujadili kazi ya usanifu na kutegemea kukamilisha kila kitu kwenye majadiliano ni kutegemea matokeo hafifu sana na jengo ambalo lina viwango duni. Kinachopaswa kufanyika sasa ili kuepuka hili kwanza na muhimu sana ni mteja na wataalamu kukaa na kupeana miongozo na mahitaji yanayohitajika kwenye jengo husika. Kisha mtaalamu ataondoka na kwenda kukaa chini akijitahidi kufanikisha kazi nzuri yenye ubora sana kisha atarudi tena kuijadili na mteja na kama itakuwa imemvutia vya kutosha ataingia kwenye kutengeneza picha za muonekano na michoro ya ramani ya mwisho.

Kwa namna hii kazi itafanyika kwa viwango bora na vya juu kwani yote yanayojadiliwa yataachwa kwa mtaalamu akatumia akili na uwezo wake kuumiza kichwa kwa vitendo na kufanikisha kufikia kile kinachohitajika badala ya watu kukaa chini na kulazimisha kujadili na kufikia hitimisho kwenye mambo ambayo hawana uwezo wala uzoefu.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *