INFINITY POOL TANZANIA (INFINITY SWIMMING POOL).
Moja kati ya vitu vinavyofanya wataalamu kwenye fani ya ujenzi katika nchi za ulimwengu wa tatu wanafanya kazi za kawaida zisizo na msisimko mkubwa ni pamoja kukosekana kwa miradi mingi ya inayojumuisha vitu kwa sababu aidha ya gharama zake au kutokuwa na umaarufu mkubwa katika mazingira husika. Sasa moja kati ya mawazo ya kipekee sana ambayo hayapatika kwa wingi sana katika mazingira ya nchi ya Tanzania lakini yenye msisimko mkubwa katika fani ya usanifu majengo ni uwepo wa bwawa la kuogelea(swimming pool) ambalo halina mwisho(infinity).
Infinity pool ni bwawa la kuogelea nyumbani, hotelini ai sehemu nyingine ambapo maji yake yanamwagika chini bila kuisha wala kuonekana kuchafuka. Muda wote yanaonekana yanatembea na kumwagika bila kuisha wala kukatika jambo linalovutia sana. Aina hii ya bwawa ndio huitwa infinity pool na huvutia sana hata kuogelea kwani maji yale huleta msisimko na mvuto mkubwa sana kuzidi bwawa la kuogelea la kawaida lisilo na uendelevu.
Karibu kwa ziada.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!