ANAYEJENGA JENGO NI MSHAURI WA KITAALAMU SIO MKANDARASI AU FUNDI.

Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikichanganya sana watu na hata kuchangia katika kupunguza thamani ya jengo ni ile hali ya watu ambao hawapo kwenye fani ya ujenzi kushindwa kujua nani ni nani katika mradi wa ujenzi. Watu wanapoona wakandarasi wana mitambo na pesa nyingi za kuendesha miradi hii wamekuwa wakidhani wakandarasi ndio wanaojenga na kusimamia kila kitu. Lakini isipokuwa tu kama mkandarasi anafanya vyote viwili lakini kazi yake kubwa kwa mfumo wa ujenzi wa toka zamani ni kutekeleza tu ujenzi lakini kazi ya kujua nini kinapaswa kujengwa na kwa namna gani ni kazi ya washauri wa kitaalamu kama vile msanifu majengo, makadiriaji majenzi, mhandisi mihimili n.k.,

Hili linajidhihirisha kwenye miradi ya ujenzi unakuta ikiwa kama mshauri wa kitaalamu hajaenda kwenye ujenzi huo kwa muda mrefu kukagua na kutoa miongozo basi utakuta mradi una makosa mengi sana ambayo yataonekana na kufanyiwa kazi kwa mujibu wa mapendekezo ya Architect. Lakini pia kwenye mradi wa ujenzi timu ya washauri wa kitaalamu huwa ndiye boss wa wakandarasi wanaofanya kazi ya utekelezaji wa mradi. Kumbuka kwamba hiyo hata michoro yenyewe inayotumika katika eneo la ujenzi imefanywa na hao wataalamu ambao pengine hawapewi heshima inayowastahili.

Hivyo wanaojenga ni watekelezaji tu wa kile ambacho kimefanywa na wataalamu kutokea site ambapo wataalamu hao pia ndio wanasimamia mradi mwingine lakini wataondola kwenye mbele tutaonana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *