NAMNA NZURI NA YA UHAKIKA YA KUTENGENEZA ARCH (NUSU DUARA) ZA UREMBO KWENYE MAJENGO.

Nimekuwa nikitembelea majengo mbalimbali yaliyojengwa na yanajengwa katika kufanya ukaguzi au kutoa ushauri kuhusu ujenzi na kukutana na changamoto na makosa mbalimbali. Makosa mengi yanatokana aidha na ujinga yaani ile mtu kushindwa kujua afanye nini katika eneo husika la ujenzi au uzembe yaani pale mtu unakuta anajua cha kufanya lakini kwa sababu mbalimbali ikiwemo tamaa au kutojali basi anakuwa hajafanya inavyotakiwa. Makosa haya mengine yamekuwa yakibakia hivyo hivyo hata baada ya ujenzi kumalizika na kupelekea ile thamani ya jengo kupungua na hivyo kwa namna moja au nyingine kutopewa hadhi ambayo ingestahili.

Sasa moja kati ya changamoto ambayo nimeona ikijirudia mara kwa mara katika kazi hizi ni watu wengi kushindwa kuseti kwa usahihi nusu duara za urembo kwenye za kwenye baraza, milango, madirisha, uwazi na maeneo mengine yote. Hili limekuwa likichangiwa zaidi na watu hao kushindwa kujua njia sahihi ya kufanya hivyo ambayo itafanya kazi kwa usahihi, ambapo mara nyingi amekuwa wakitumia Kamba au kupima kwa macho yao tu bila kutumia mwongozo mwingine wowote ule. Hilo limekuwa likipelekea nusu duara hizo maarufu kama arches kukosa usahihi kwa kuwa na mawimbi mawimbi au mkunjo wa nusu duara ambao haujanyoosha hivyo mwonekano wake kuwa na mapungufu ya ubora wa kiufundi(poor workmanship).

Kwa hiyo moja kati ya njia nzuri unazoweza kuwa unatumia katika kuipata nusu duara hiyo ni kutumia bomba za umeme maarufu ambazo kutaalamu ni maarufu zaidi kama “conduit pipes”. Bomba hizi za umeme kwanza zina wastani mzuri wa ukubwa au saizi nzuri kwamba sio pana au nene sana wala sio nyembamba sana bali zina wastani mzuri wa saizi kuweza kutumika kwa ajili ya zoezi hilo. Pili zina uimara wa kutosha kuikunja ikakunjika kwa usawa kupata kile ile nusu kipenyo unayohitaji kwa kiasi unachohitaji kwa kuikunja kwa kiasi hicho na bila kupoteza usahihi wake inakupatia ile nusu duara utakayo kama ulivyo kwa kadiri ya ukubwa wake.

Unachofanya wewe sasa baada ya hapo ni kuichorea kwa kutumia chaki au mkaa katika ile marine board au mbao iliyowekwa kwama form kwa ajili ya kuipata arch hiyo ambapo kwa kuwa bomba ya conduit pipe hukunjika kwa ushahihi mkubwa utaipata hiyo arch katika mstari wa duara sahihi sana. Ukishakamilisha kuchora mstari huo ndipo unakuja kuweka na kupigilia zile mbao za “plywoods” zinazowekwa kama formworks ya kupata hilo umbo la arch ambapo hizo “plywoods” zinalazimika kufuata ule mstari uliochorwa kwa umakini na usahihi mkubwa sana kuhakikisha haibomoki wala kuhama kwenye mstari huo unaoelekea kutupatia arch iliyonyooka kama mstari wenyewe.

Kisha baada ya hapo ni kuimarisha mfumo mzima wa formworks husika na kumwanga zege hilo ambalo litaleta mwonekano mzuri sana. Ikiwa unapitia changamoto za kwenye eneo hili au kuna mtu unayemfahamu anayepitia changamoto hiyo unaweza kutujulisha.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *