CHANGAMOTO KARIBU ZOTE ZA KWENYE JENGO ZINATATULIKA.

Majengo kama ilivyo katika maeneo mengine yote na kwenye fani zote huwa yanachakaa na mitindo yake pia kupitwa na wakati kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele na mabadiliko zaidi. Katika tasnia ya usanifu majengo na ujenzi mabadiliko ya kiteknolojia yanayopelekea mitindo mipya ya majengo pamoja na vifaa vya ujenzi yameathiri sana tasnia hii hususan kwa namna chanya. Lakini hilo sasa limepelekea majengo ya zamani au hata ya miaka zaidi ya kumi iliyopita kuwa tayari yamepitwa na wakati au kwa namna moja au nyinyine hayako katika viwango vya mitindo mipya inayokuja sambamba na vifaa vya kisasa zaidi vya ujenzi.

House improvement concept. Rear view of Asian construction worker looking away.

Kinachotokea ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao waliojenga miaka iliyopita na wanaona sasa kuna mambo mengi mazuri ya sasa na wangetamani majengo yao yawe katika mitindo na viwango vya sasa lakini hawajui au hata hawajafikiria kama wanaweza kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba kwa namna yoyote ile ambayo teknolojia ya ujenzi imefikia sasa hivi tunaweza kubadili jengo lolote lile kuanzia ndani yaani mzunguko wa ndani mwonekano wa jengo zima kwa nje kuwa la kisasa kabisa na linaloendana na teknolojia ya sasa bila kujali ni la zamani kiasi gani. Hakuna wasiwasi wowote juu ya hili na linawekana kabisa kufanyika katika usahihi na viwango vya juu kabisa kwa namna yoyote ile.

Hilo linawezekana kabisa iwe ni kuongeza ukubwa wa jengo na vyumba au kuboresha muonekano wake au kuongeza na kupunguza milango na madirisha au kipengele kingine chochote ndani ya jengo. Kuna uwezekano pia wa kuweka mifumo mipya mbalimbali ndani ya jengo na kuondoa ile ya zamani na ikafanya kazi vizuri sana. Hilo linawezekana pia hata kama ni nyumba ya kawaida ya chini kubadilishwa kuwa ghorofa au hata ghorofa kuongezewa zaidi kwenda juu.  Suala la kufanya mabadiliko ya jengo la aina yoyote kulifanya la kisasa au kulipeleka kwenye matumizi mengine yoyote kutokea yale ya awali ni kazi ya kufanya inayowezekana kufanyika kwa umakini mkubwa na kwa usahihi mkubwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *