KAZI YA KUFANYA MAHESABU YA UJENZI NI YA MTAALAMU WA UKADIRIAJI MAJENZI.
Mara nyingi katika kazi tunazofanya tumekuwa tunakutana na wateja ambao wanahitaji kufanyiwa kazi za michoro ya ramani kisha baada ya hapo wanahitaji kufanyiwa kazi za ukadiriaji wa gharama za ujenzi wa majengo ambapo wanategemea wewe mwenyewe ndio ufanye kazi hiyo. Licha ya kwamba ni kweli kwamba mtaalamu wa usanifu majengo au uhandisi mihimili anaweza kupitia uzoefu kutengeneza mahesabu yasiyo rasmi ya gharama za ujenzi lakini kitaaluma hiyo sio fani yake wala hana ujuzi sahihi kwa kazi hiyo, hivyo hawezi kuifanya kwa usahihi na kwa kuzingatia kanuni zake vile inavyotakiwa.
Kwa bahati mbaya zaidi watu wanaohitaji kufanyiwa kazi hiyo hufikiria kwamba hiyo ni sehemu ya kazi ya michoro ya ramani za ujenzi au ni kazi inayotakiwa kwenda sambamba au pamoja na hiyo. Sasa hilo sio kwamba tu sio kweli bali sio fani yake kabisa na anapofanya kazi hiyo mara nyingi kuna vitu vinavyoweza kukosekana vinatakavyokuja kuonekana baadaye wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Kazi ya kufanya makadirio ya ujenzi ni taaluma iliyokamilika inayosomewa kwa miaka minne katika ngazi ya shahada ya kwanza chuo kikuu.
Hivyo kwa mteja ambaye anahitaji kupata nyaraka ya makadirio ya ujenzi iliyofanyika kitaaluma na inayoweza kutegemea kutumika kama nyaraka rasmi katika eneo hilo anapaswa kutafuta mtaalamu wa ukadiriaji majenzi anayejulikana kitaalamu kama Quantity Surveyor au kwa kifupi (QS). Mkadiriaji huyu wa majenzi atafanya kazi hiyo kwa urahisi zaidi na kuweza kutoa maoni na mapendekezo bora zaidi ya matazamio ya mradi husika kwa upande wa gharama na ubora na thamani inayoletwa na gharama hiyo(value for money). Hata hivyo itakuwa busara na kimsingi ni muhimu sana kutafuta mtaalamu wa namna hiyo mwenye uzoefu na anayeijua kazi yake Barabara ili kuepusha kufanyika kwa kazi duni iliyo chini ya viwango.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!