SIO LAZIMA UBOMOE NYUMBA YAKO YOTE ILI KUJENGA NYINGINE UNAWEZA KUIUNGANISHIA.

Watu mbalimbali huwa wanapewa nyumba za urithi au kununua eneo ambalo tayari kuna nyumba ndani yake hivyo anakuwa amenunua eneo hilo pamoja na nyumba hiyo. Baada ya uwezo wa kifedha kuongezeka na shauku ya kujenga nyumba bora nzuri na ya kisasa kujenga hamasa huamua kubomoa nyumba hiyo ili kujenga nyumba nyingine mpya kabisa eneo hilo. Wakati mwingine nyumba inayobomolewa huwa ni nyumba imara sana na iliyojengwa kwa ubora wa hali ya juu hivyo kuwa katika hali ambayo ingeweza kuwa msingi imara wa nyumba nyingine ikiwa itatunzwa. Lakini kwa sababu ya kukosekana kwa maarifa na ushauri wa kitaalamu nyumba yote hubomolewa.

Hata hivyo kulingana na ubora wa nyumba hiyo na pengine kuhifadhi kumbukumbu kutokana na umuhimu wa kihistoria wa nyumba husika, huwa sio lazima nyumba yote kubomolewa bali inaweza kuboreshwa na kuongezewa kwa kuunganishiwa nyumba nyingine ya kisasa kwa hapo hapo ilipo. Nyumba hii itakapoongezewa inaweza kuwekewa vyote vinavyohitajika na kuongezewa kwa kujumuisha vile vilivyokuwepo kwenye nyumba ya zamani kwa kubadilisha baadhi ya matumizi ya vyumba na mpangilio kubadilishwa na kuboreshwa lakini bila kuondoa yote moja kwa moja. Jambo la kwanza litakalofanyika ni kutengeneza ramani iliyoongeza maboresha na ukubwa zaidi wa jengo hilo kuanzia kwenye msingi, nyumba mpaka kupaua.

Mwisho wa siku unakuwa umepata jengo lile la kisasa ulilokuwa unalitaka bila kubomoa nyumba yote kitu ambacho kinakuwa kimekusaidia hata kuokoa gharama za kujenga kwani kuna baadhi ya maeneo yanakuwa yalikuwa tayari kutegemea na ukubwa ulioongezeka kutoka kwenye nyumba ya awali. Baada ya michoro kukamilika ndipo ujenzi wake unaanza. Hata hivyo ni muhimu sana kwa ujenzi wa aina hii kuhakikisha unafanyika chini ya usimamizi madhubuti sana ya mtaalamu aliyechora kwani uwezekano wa kufanya makosa yatakayoligharimu sana jengo ni mkubwa ikiwa mradi hauna usimamizi wa mtaalamu kiongozi aliyebobea. Hivyo ikiwa una jengo ambalo usingependa kulibomoa moja kwa moja iwe ni nyumba ya kawaida au ni ya ghorofa ni muhimu kuchukua njia hii mbadala.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.   

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *