UNATUMIA NJIA GANI KUKAGUA UBORA WA JENGO LAKO IKIWA UMEMPA MKANDARASI MKATABA WA JUMLA?

Kuna maswali huwa najiuliza kuhusu namna ujenzi unafanyika na yananiletea tena maswali zaidi. Watu wengi huwapa watu au makampuni mbalimbali kazi za kuwajengea majengo yao au nyumba zao mkataba wa jumla kwa maana ya kusambaza vifaa na ufundi kwenye jengo au kwa maana ya kila kitu kwa imani waliyoijenga kwao lakini wengi hawana mfumo au utaratibu wa kukagua kujihakikishia kama kweli kazi imefanyika kwa viwango na usahihi na badala yake wanakubaliana na chochote watakachokabidhiwa. Hii imekuwa ni moja ya sababu ya asilimia kubwa sana ya kuvunjika kwa mahusiano baina ya mteja na mkandarasi mara baada ya mradi kumalizika.

Hata hivyo ili kupata kazi sahihi na iliyojengwa kwa viwango basi haipaswi mradi kukaguliwa ukiwa umemalizika pekee bali kuna hatua nyingi muhimu kuanzia mwanzo mradi unapoanza na mchakato mzima kuendelea mpaka mradi kumalizika na kukabidhiwa mteja. Mteja anachotakiwa kufanya ni kuwa na mtaalamu wa ushauri wa kitaalamu ambaye naye atakuwa na muongozo maalum wa kile anachokwenda kukagua katika jengo hilo na ndiye atakayeleta ripoti yote ya maendeleo ya jengo na ikiwa jengo linajengwa kwa viwango na kwa usahihi unaotakiwa.

Mshauri huyu wa kitaalamu anapaswa kuwa analinda maslahi ya mteja muda wote dhidi ya wale ambao mteja amewaamini na kuwa kazi. Hivyo baadaye wakati wa kukabidhiana basi yanaangaliwa yale mambo ambayo yalipaswa kufikia viwango bora na ndio yanayotumika kuhukumu kazi hiyo na kuikabidhi rasmi kwa mteja ikiwa imekamilika. Hivyo mteja anapaswa kutafuta mshauri wa kitaalamu kumsaidia kumhakikishia kwamba kazi imefanyika vizuri na kwa usahihi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *