MOJA KATI YA MBINU ZA KUDHIBITI WIZI WA VIFAA VYA UJENZI WAKATI UNAFANYIKA.

Moja kati ya kilio kikubwa cha wateja na hata wakandarasi wengi kwenye miradi ya ujenzi inayokuwa inaendelea ni suala zima la wizi katika maeneo ya ujenzi. Tatizo la wizi ni sugu sana na kwa sababu kwenye miradi ya ujenzi kuna watu wengi wasio na nafasi za juu wala elimu kubwa wala malengo yoyote makubwa kwenye maisha au waliopevuka wanaofanya kazi kwenye miradi hii basi wizi wa vifaa na vitu vingine umekuwa ni kitu kilichozoeleka sana na ni kilio kisichoisha. Ikiwa mtu hutakuwa makini na mbinu nzuri za udhibiti kwenye eneo lako la ujenzi basi kuibiwa hakuepukiki.

Hata hivyo lakini pamoja na kuwepo kwa changamoto hii kubwa ya wizi ambao unaweza kufanywa hata na mtu unayemwamini sana bado jukumu la kujilinda usiibiwe ni jukumu lako mwenyewe. Unaweza kulalamika sana au kulaumu sana na hata kukasirika sana lakini bado hilo halitaweza kubadili tabia za watu ambao hata sio rahisi kufahamu kwa haraka tabia zao kiundani na bado hupaswi kutumia hilo kama kisingizio cha kuhalalisha kuibiwa ambako kwa sehemu ni uzembe wa kukosa mikakati sahihi ya kudhibiti hilo. Unapaswa kufahamu changamoto hiyo na kuanza kujipanga mapema kuikabili kabla haijakuathiri na kuleta madhara hata kwenye mradi.

Sasa leo nataka nikushirikishe moja kati ya mbinu hizo za kudhibiti wizi na ubadhirifu kwenye eneo la ujenzi. Mbinu hiyo ni kumfanya kila anayeingia kwenye eneo la ujenzi kuwa shushushu wa wenzake wote sambamba na kufanya ziara za kushtukiza katika eneo la ujenzi mara kwa mara na kuhakikisha umefukuza kazi mtu ambaye amekutwa na tabia zisizotakiwa. Mbinu hii ya ziara ya kushtukiza ambayo utaifanya kwenye miradi ya ujenzi wenye mfumo wa mashushushu wanaoripoti kwako kila mmoja kivyake itakurahisishia sana kazi kwa sababu kwanza kutakuwa na umakini sana katika eneo la ujenzi na wewe utapata taarifa nyingi sana zitakazosaidia kujua namna ya kukabiliana na changamoto za wafanyakazi zinazoendelea katika eneo la ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *