NAANDIKA KUTOKA KWENYE UZOEFU BINAFSI.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu makala zinazokwenda hewani hapa kwenye tovuti zinaandikwa kutoka kwenye chanzo gani cha taarifa. Ni kweli kwamba hizi makala bado zinaendelea kuja sana tena zinaongeza kasi ya ujio wake japo tunataka kuziboresha zaidi ili ziwe zinagusa sana watu kwa namna zote hizi tofauti. Hata hivyo makala hizi zinaandikwa kutoka kwenye uzoefu binafsi wa mwandishi mwenyewe wa ujenzi kupitia matatizo na changamoto anazokutana nazo kila siku anaposhughulika na kazi hizi kuanzia katika hatua ya ushauri wa kitaalamu na michoro mpaka kujenga kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Mwandishi amekuwa akikutana na changamoto hizi mara kwa mara na kwa namna tofauti tofauti na kwa kuliona hilo ameona kuliko kuzungumzia tu kwa watu na kunung’unika, kama anavyosema mwenyewe ni uache kulalamika na kufanyia kazi au kurekebisha kile ambacho ni changamoto au ukae kimya. Sasa kuandika kwanza maudhui haya yanaendelea kuongeza thamani kwa watu kwa namna mbalimbali, hivyo na kadiri anavyoendelea kukutana na changamoto nyingi zaidi ndivyo maudhui haya yanavyoendelea kupatikana bure kabisa kwa wingi zaidi kusaidia watu matatizo mbalimbali madogo na makubwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *