KUBOMOA NYUMBA NA KUYATUMIA TENA MABATI AU VIGAE VYA NYUMBA YAKO.

Mara nyingi watu wamekuwa aidha wakibomoa nyumba au wakiendeleza nyumba au kukarabati nyumba kwa namna ambayo inahusisha kuondoa kwanza bati za nyumba hiyo. Kuondoa huku bati au malighafi nyingine iliyotumika kutengeneza paa kama vile vigae kumekuwa kunadhaniwa na watu wengi kwamba inalazimu mtu aweke paa jingine jipya kabisa kwa kuwa lile linakuwa limeshaharibika. Kwa mfano mtu ambaye nyumba yake ni ya kawaida isiyo ya ghorofa kisha mtu huyo anahitaji kuifanyia mabadiliko ya michoro ya ramani na kuiendeleza kuwa ghorofa ambapo ni lazima itahusisha kuondoa paa na kumwaga jamvi la zege ya sakafu ya kwanza ili kuendelea juu.

Kwa kesi hiyo wengi hudhani kwamba bati au vigae vinavyokwenda kuondolewa ili kupisha mwendelezo wa ghorofa ni vya kutupa na kununua upya vingine. Hili limekuwa likiwaumiza watu hasa ambao walitumia gharama kubwa kununua bati au vigae vya gharama ya juu kwa kuthamini nyumba zao kuona kwamba wanakwenda kuvipoteza wakati ambapo bado ni vizima kabisa na vina maisha marefu sana mpaka kuja kuharibika. Wakati mwingine hili limekuwa likiwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye kupenda muonekano wa nyumba zao kwenye mapaa kiasi cha hata kuahirisha mpango huo au kuamua kwenda kujenga upya nyumba ya kuishi katika eneo jingine.

Habari ni njema ni kwamba unaweza kuondoa paa la aina yoyote vizuri na kwa umakini mkubwa kisha kuweza kulitumia tena katika nyumba hiyo hiyo au nyingine. Kwa mfano umeamua kubadilisha nyumba yako kutoka kuwa nyumba ya kawaida kuelekea kuwa nyumba ya ghorofa ambapo unalazimika kuondoa paa ili kupisha mwendelezo wa sakafu nyingine ya juu unaweza kufanikisha hilo. Unaondoa vigae au bati lote kwenye paa na kuhifadhi pembeni kisha kujenga kuelekea ghorofa ya kwanza na unapofikia kupaua unatumia vigae au bati zile zile katika kuezeka. Hili tumefanya mara kadhaa na kufanikiwa kwa karibu asilimia mia moja. Isipokuwa tu kama wewe mwenyewe umeamua kubadilisha paa lakini hupaswi kuwa na hofu kabisa ya kuogopa kwamba unakwenda kuingia gharama nyingine ya kununua bati au vigae kwani vitatumika vile vile vilivyoondolewa kwa umakini mkubwa na kuhifadhiwa vizuri.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *