GHARAMA ZINAZOONGEZEKA KWENYE UJENZI.

Katika jambo lolote lile kwenye maisha huwa ni vigumu mtu kutabiri kila kitu kitakachotokea katika safari nzima ya kulifanya na kukamilisha jambo husika. Kuna dharura mbalimbali ambazo hazikufikiriwa kabisa mwanzoni huweza kutokea na kuathiri jambo husika kwa namna nyingi kuanzia muda, gharama na hata uelekeo wa jambo hilo. Hili limepelekea kwamba watu makini wanapokuwa wanapanga utekelezaji wa jambo kuweka uwezekano huu wa dharura kutokea baada ya aidha kubashiri kutokana na uzoefu au kuwa na kiwango ambacho ni cha makadirio ya jumla.

Kwenye miradi ya ujenzi napo mambo hayapo tofauti na hapo, kwani licha ya wataalamu wote kukaa chini kutengeneza mpango kazi wa mradi sambamba na gharama zake lakini bado kuna hali nyingi zisizotabiriki kiurahisi hutokea kwa namna mbalimbali, nyingine zikiwa ni za asili na nyingine zikitokana na maamuzi mbalimbali ya watu. Hali hizi zisizotabirika zinaweza kuwa ni mabadiliko ya hali ya hewa, majanga ya asili, mabadiliko ya sera za serikali, kukutana na miamba migumu chini ardhini, kukutana na mawe makubwa, kukutana na aina tofauti ya udongo iliyotarajiwa mwanzoni, kukutana na mashimbo makubwa n.k., Vyote hivyo vinaathiri sana gharama za mradi na kusababisha ongezeko la gharama ambalo halikuweza kutazamiwa au kutarajiwa wakati wa kufanya makadirio ya mradi husika.

Hivyo katika makadirio ya gharama hizo za ujenzi huwa kuna ongezeko la gharama ambalo huitwa kwa jina la kitaalamu “contingency” ambalo hukadiriwa kwa kutumia uzoefu wa taaluma ya ukadiriaji majenzi na mradi husika. Gharama hizi za makadirio huweza kuwa chini au juu kadiri ya aina na mazingira ya mradi wenyewe, hata hivyo karibu mara zote miradi ya aina zote iwe ni ya watu, binafsi, taasisi binafsi na hata mashirika ya kiserikali huwa haikosi ongezeko la gharama japo wakati mwingine huweza kuwa ni kidogo. Gharama hizi huwa ni rasmi na hufidia dharura zote ndogo ndogo na hata wakati mwingine kubwa zilizojitokeza kwenye mradi husika wa ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *