SEHEMU KUBWA YA MAKOSA KWENYE UJENZI YANAREKEBISHIKA

Kutokana na kukosa uzoefu kwa pande zote mbili yaani upande wa mteja na upande wa mtaalamu anayejenga huwa inatokea kwamba baadhi ya miradi ya ujenzi inakuwa na makosa makubwa sana wakati mwingine, makosa ambayo yanaweza kuwa hayafai hata kuvumilika au yanaweza kuvumilika kimatumizi lakini yakawa ni vigumu kuvumilika kwa taswira mbaya na aina ambayo yanaleta kwenye jengo husika. Kwa kesi ya namna hii basi mhusika analazimika kufanya marekebisho ya uharibifu uliofanyika ili kulirudisha jengo kwenye hadhi yake liweze kuwa na thamani iliyokusudiwa na ambayo itawashawishi watumiaji kwamba ni jengo lenye thamani linayopewa.

Ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya makosa yanayofanyika kwenye jengo yanaweza kurekebishwa, japo wakati mwingine hilo huweza kuhusisha gharama kubwa sana kutegemea na kiwango cha makosa pamoja na aina ya makosa. Habari njema ni kwamba sio lazima mtu uhangaike kurekebisha makosa yote kwa pamoja hasa ikiwa yanakuja na gharama kubwa, bali unaweza kurekebisha kwa hatua kwa kwenda taratibu taratibu mpaka kukamilisha kipengele kimoja na vingine kuelekea kukamilika. Jengo linaweza kurekebishwa kuanzia kwenye mpangilio wa kisanifu, nafasi za ndani, maeneo yenye uwazi, mwonekano, mifumo ya mihimili, mifumo ya huduma za ndani ya jengo n.k.,

Kurekebishwa kwa makosa husaidia jengo kufanya kazi kwa ufanisi na ubora na kurudisha thamani ambayo itafanya watu makini wenye kuangalia thamani na hadhi kuwa tayari kulitumia jengo hilo na hata kulipia gharama kubwa ikiwa ni jengo la biashara. Lakini hata kwa jengo la makazi likiongezewa thamani kwa kufanyiwa marekebisho yanayohitajika basi litafurahiwa sana na watumiaji ambao wataona kwamba jengo hilo ni la kipekee na lenye thamani kubwa. Hivyo unapokuwa umejenga jengo lenye makosa, iwe ulijua au ulikuja kugundua baadaye wakati wa kutumia basi jua kwamba una nafasi ya kulifanyia marekebisho likaongezeka thamani na ukalipenda sana. Karibu sana kwa ushauri zaidi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *