GHARAMA ZA UJENZI HAZIKO KWENYE TOFALI.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa binadamu walio wengi kuhukumu vitu kwa kuangalia jinsi vinavyoonekana kwa nje. Muonekano umekuwa ndio kipimo cha vitu kwa sababu ya watu kutokuwa na uelewa wa haraka juu ya undani wa mambo mbalimbali. Hivyo watu wamekuwa wakipima kila kitu wasichokijua kiundani kutokana na muonekano wake. Jambo hilo halijaenda tofauti sana kwenye tasnia ya ujenzi ambapo watu kwa kutokujua wanapima gharama kwa muonekano wa nje wakifikiri wanachokiona ndicho chenye gharama kubwa.

Mara nyingi utakuja mtu anauliza zitaingia tofauli ngapia katika nyumba yangu, na bati zitaingia ngapi katika nyumba hiyo kisha anauliza gharama ya tofali moja ni kiasi gani na bati ni kiasi gani. Yeye kwa Mawazo yake anajua tofali na bati ndizo zenye gharama kubwa. Hata hivyo watu wasichojua ni kwamba moja kati ya vitu vinavychukua gharama kidogo kwenye mradi wa ujenzi ni pamoja na tofali. Gharama za tofali wakati mwingine huwa mpaka chini ya asilimia 10% ya gharama za vifaa vyote vinavyotumika kwenye ujenzi huku kukiwa na maeneo mengine mengi yanayochukua gharama kubwa kuliko tofali.

Kwa mfano maeneo yote ya jengo ambayo yanajengwa kwa zege ni moja kati ya maeneo yanayochukua gharama kubwa sana hasa zege hilo linapokuwa na nguvu ndani yake. Saruji nayo inapotumika kwa wingi inagharimu fedha nyingi sana pia. Upauaji wa nyumba nao ni kati ya maeneo yanayochukua gharama kubwa sana huku umaliziaji wa nyumba ikiwa ndio eneo linachukua gharama kubwa zaidi kuliko zote. Kimsingi gharama ya umaliziaji wa nyumba huchukua karibu au zaidi ya nusu ya gharama ya ujenzi wote kwa ujumla ikijumuisha na hizo tofali zenyewe.

Hivyo pale mtu unapofikiria gharama za ujenzi badala ya kukaa na kuwaza kuhusu idadi ya tofali na bati na bei zake ni vyema kumtafuta mtaalamu ukamshirikisha malengo yako hayo ya kufanya ujenzi wako kisha mkajadili gharama kujua wapi utaanzia na wapi ni kwa kuwekewa uzito zaidi. Hilo litasaidia mtu kuelewa uhalisia wa kile unachokwenda kufanya na hivyo kukamilisha kwa uhakika zaidi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *