GHARAMA ZA UJENZI NI ZILE ZILE.

Ukishakuwa ni mtu unayehusika na mambo ya ubunifu, usanifu na uhandisi wa majengo basi unapotembea kila mahali hususan kwenye miji mikubwa na kwenye makazi ya watu macho siku zote yanaangalia mazingira yanavyojengwa na aina mbalimbali za ubunifu uliofanyika. Katika kufanya hivi mtu unaweza kuona jinsi kuthamini na kulipia utaalamu kunavyoendelea kuongeza thamani ya majengo na kuboresha mazingira na maisha ya watu kwa ujumla. Hata hivyo kati ya vitu ambavyo huwa vinasikitisha sana katika kutupia macho kazi za kibunifu zilizofanyika ni kukutana na majengo mengi ambayo yamefanyika kiholela na kukosa ubunifu na hivvyo thamani yake kuonekana wazi kwamba iko chini na hivyo jengo zima kwa ujumla kukosa thamani na hadhi ambayo lilipaswa kuwa nayo.

Sasa kinachosikitisha zaidi sio tu kwa sababu jengo limekosa ubunifu na hivyo thamani yake na hadhi yake kushuka bali pia ni gharama ambayo jengo hilo limeingia licha ya kufanyika kiholela na hivyo kukosa hadhi. Gharama ambayo inatumika kujenga jengo lililokosa ubunifu na hivyo thamani na hadhi yake kushuka ni ya wastani huo huo inayotumika kujenga jengo bora lenye mvuto kwa ubunifu uliotumika na kupelekea thamani na hadhi yake kuwa juu. Yaani kinachokuwa kimetokea ni kwamba pesa nyingi zimetumika kwenye ujenzi ambao thamani ya kazi yake ni ubunifu iko chini sana kwa hiyo inakuwa ni hasara kubwa kwa upande wa mteja kwa kushindwa tu kufanya maamuzi sahihi.

Hivyo kwa kuwa watu wengi hukwepa vitu vyenye thamani kubwa zaidi kwa sababu ya kuogopa gharama hapa hawapaswi kuogopa kwa sababu wastani wa gharama ni ule ule, lakini changamoto ni kwamba makosa hufanyika kwenye kufanya maamuzi sahihi ya watu wa kufanya nao kazi hususan mwanzoni kabisa mwa mradi. Watu wanapaswa kuondokana kabisa na hofu ya kufanya kazi nzuri kwa kuhofia gharama kwani kazi inaweza kuwa nzuri sana hata kwa wastani huo huo tu wa gharama. Jambo la msingi la kuzingatia ni kutafuta washauri sahihi wa jengo lako au mradi wako wa ujenzi ambao wana taaluma husika, uwezo na uzoefu wa kazi katika eneo la ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi kwa ujumla kisha kufanya nao kazi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *