AMUA KWA USAHIHI KUHUSU MRADI WA UJENZI WA NYUMBA YAKO.

Watu wa zamani maarufu zaidi kama “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ukweli ni kwamba mara nyingi watu huwa hawaoni uzito wa jambo au changamoto kwa kuisikia tu kwa maneno kama bado haijawatokea na ndio maana mambo yanapokwenda vizuri watu huchukulia kawaida na mara nyingi huwa hawashukuru wala kuonyesha kujali sana vile mambo yamekwenda vizuri. Inapotokea sasa mambo yanapokuwa yamekwenda vibaya basi watu ndio sasa huanza kupaniki, kuogopa na kujaribu kufikiria kwa makini kuwa walikosea wapi. Hii ni licha ya kwamba alikuwa akiimbiwa na kutahadharishwa juu ya hatari zote ambazo anaweza kukutana nazo mbele ya safari. Jambo hili hutokea mara kwa mara na watu kuishia kusema laiti ningelijua.

Sasa ili mtu kuepuka au kupunguza majuto katika maisha yako ni muhimu sana uwe unachukua tahadhari mara zote lakini pia uwe unajikumbusha uwezekano wa mambo mabaya ambayo yataweza kutokea au yangeweza kutokea na kuyavuka kisha kushukuru sana kwamba umeweza kukwepa risasi iliyokuwa inakulenga kichwani. Unapaswa kuwa na muda wa kutafakari yote yanayotokea na kushukuru kwamba uko pazuri kisha kuongeza bidii na umakini kwa yale yanayoelekea kuja mbele yako. Lakini pia ni muhimu sana sasa kuhakikisha unachukua ushauri sahihi kutoka kwa wazoefu, wabobezi na wataalamu katika eneo husika ambao watakupa mwongozo na kukuongoza njia kukwepa kufanya makosa na hivyo kufanya maamuzi sahihi kila unapofikia wakati wa kufanya maamuzi muhimu.

Katika ujenzi mara nyingi kuna majuto mengi ambayo yatakuja baadaye yatakayotokana na wewe kutokujua baadhi ya mambo muhimu kwenye ujenzi kwa ujumla kuanzia mwanzo kabisa wakati wa kuandaa ramani ya jengo lako. Majuto hayo yanaweza kuwa makubwa sana kwa sababu unakuta sio rahisi tena kufanya mabadiliko au mabadiliko yatakayogharimu fedha nyingi sana au majuto hayo yanaweza kuwa sio makubwa sana kwa sababu kuna nafasi ya kufanya mabadiliko yasiyohitaji gharama kubwa. Sasa ili kukwepa au kupunguza majuto inafaa kabla ya kuanza mradi wako wa ujenzi ufanye maamuzi sahihi ya kutafuta ushauri kutoka kwa wazoefu, wabobezi na wataalamu watakaokuongoza njia na kukupa njia mbalimbali mbadala kila unapofikia wakati wa kufanya maamuzi muhimu.

Hivyo usahihi wako wa maamuzi katika ujenzi utakuja katika eneo la kutafuta ushauri wa kitaalamu na ushauri wa watu wazoefu ambao watakupa siri nyingi za kukabiliana na changamoto ngumu na nzito hasa za kudili na watu katika mradi wako wa ujenzi. Utafanya makos ana kuingia kwenye majuto sana kama utaenda mwenyewe moja kwa moja kwenye kufanya maamuzi muhimu bila kushirikisha na kuhitaji ushauri kutoka kwa watu mbalimbali.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *