CHANGAMOTO MBILI SUGU ZA KWENYE MIRADI YA UJENZI.

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ikiwa mtu atafuata taratibu zilizowekwa ambazo zinahitaji mtu yeyote anayetaka kufanya mradi wa ujenzi kuzingatia mchakato mzima kuanzia kwenye zoezi la zabuni katika kupata washauri wote elekezi wa kitaalamu kwenye ujenzi kisha kupata mkandarasi baada ya zoezi la kukamilika kwa hatua za awali eneo la ushauri wa kitaalamu yaani michoro basi mtu huyo ana nafasi kubwa sana ya kukwepa changamoto hizi.

Lakini katika uhalisia ni mara chache sana watu hupitia mchakato huo uliowekwa kisheria katika kuhakikisha kazi au miradi ya ujenzi hasa miradi mikubwa inafanyika kwa kuzingatia ufanisi na ubora unaokubalika. Hili huwa halifanyika kwa sababu kadhaa kwanza watu au wateja wenye miradi kutokufahamu kwa undani juu ya utaratibu huu au kukwepa mchakato mzima kwani unahusisha watu wengi na unachukua muda kukamilika, hivyo kama mtu ahitaji usumbufu wa kudili na watu wengi au kama mtu ana haraka sio rahisi kujihangaisha na mchakato wote huu. Hivyo sasa anakuwa hawezi kukwepa changamoto za aina hii.

Changamoto mbili sugu sasa kwa miradi mingi ya ujenzi hasa miradi midogo na ya ukubwa wa wastani ni udanganyifu/ubadhirifu na ubora. Suala la wizi na ubadhirifu wa katika miradi ya ujenzi ni kama utamaduni hasa kwa mafundi au watu ambao wanaendesha miradi yao bila kuwa na taasisi au mifumo ya udhibiti. Changamoto nyingine ni ubora ambao nao unapaswa kudhibitiwa kwa kuhusisha wataalamu wenye uzoefu na uwezo katika taaluma husika iwe ni usanifu wa jengo, uhandisi mihimili, uhandisi umeme, uhandishi huduma n.k., Lakini pia wizi na udanganyifu huchangia sana katika kukosekana kwa ubora wa jengo kwa sababu ya uchakachuaji wa vile viwango vilivyowekwa.

Hivyo sasa ili kupambana na changamoto mtu unapokuwa unataka kufanya mradi wa ujenzi ila kufuata utaratibu huo mrefu na unaohusisha wataalamu wengi ambao ni wa uhakika basi angalau unapaswa kufanya kazi na mtu au taasisi ndogo inayoendesha mradi wa ujenzi kwa kutumia mifumo imara ya udhibiti katika hatua zote za utekelezaji wa mradi wa ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *