HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJENGA NYUMBA YA NDOTO YAKO.

Licha ya kujitahidi kutafuta sana maisha lakini watu wengi hushindwa kujenga nyumba za ndoto zao kwa sababu hushindwa kujua kwamba mradi wa kufanikisha kujenga nyumba ya ndoto yako unahitaji umakini mkubwa na kuna maeneo ya muhimu yanayopaswa kuzingatiwa lakini muhimu sana ni kupata mtu sahihi, mwenye uwezo na uzoefu wa kukuongoza kwa usahihi. Jambo hili hupelekea watu kupoteza pesa nyingi baada ya kukosea mwanzoni wakijaribu kurekebisha makosa yao nabado mara nyingi hushindwa kufanikisha kwa usahihi kile walicholenga kwa sababu kurekebisha makosa yote huhitaji gharama kubwa sana sawa na kuanza mradi upya kitu ambacho wengi wanakuwa hawana tena uwezo wa kumudu hilo.

Wakati mwingine watu hujuta sana na kuumia sana kiasi cha kushindwa hata kuendelea na mradi husika na aidha kuutelekeza au kuamua kuuza kabisa eneo hilo na kwenda kuanza upya sehemu nyingine wakiwa wameshapoteza muda na fedha. Hata hivyo kwa wengi ambao huhakikisha wamefuata taratibu tunazowashauri hufurahia nyumba zao na mazingira yao kiasi cha kujitahidi kununua maeneo ya Jirani ili kuongeza eneo lake na kuboresha zaidi mazingira na mandhari yaliyomzunguka ambayo humvutia sana. Yuko dada mmoja maeneo ya Mbezi Beach, Afrikana, Dar es Salaam alikuwa anajenga nyumba ya ndoto yake lakini alifeli kwenye kuchagua watu sahihi wa kufanikisha hilo. Yeye mwenyewe anadai kwamba kosa hilo lilipelekea yeye kupoteza zaidi Tshs milioni 50 kwenye marekebisho na bado hakuweza kurekebisha kila kitu. Tuliweza kumsaidia kupambana kurekebisha maeneo mengi kupitia kwa kuzingatia kanuni za kitaalamu ambazo hazikuzingatiwa katika utekelezaji wa mradi huo.

Baada ya kuifanyia marekebisho kutoka ilikokuwa imeharibiwa sana na mkandarasi aliyepita imeweza kupendeza kiasi kwamba wageni wengi wanaomtembelea wanaisifia sana.

Hivyo kujenga nyumba ya ndoto yako, tutakufanyia kazi nzuri sana ya design na picha za kiasasa, na kuijenga kwa viwango bora kama ilivyo kwa namna tulivyoifanya, tupigie sasa ambapo tuna punguzo la asilimia 30% wakati huu mwanzoni mwa mwaka ambapo pia tumeshusha gharama za ujenzi mpaka 30% unufaike na ofa hii. Fanya hivyo kwa kuwasiliana na sisi kwa namba za simu hapa chini kuweza kuchukua hatua mara moja.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *