FANYA HIVI KUEPUKA KUIBIWA KWENYE UJENZI.

Watu wengi wameumizwa sana kwenye ujenzi kiasi kwamba kila wanapopanga kufanya mradi wa ujenzi wanafikiria mara mbili kwanza ni lini atapata nafasi asimamishe shughuli zake zote akasimamie mradi wake wa ujenzi ili kuepusha kuibiwa na kuharibiwa kazi. Hata hivyo bado kusimamia mwenyewe sio suluhisho kamili la kuepuka kuibiwa kwani mafundi wengi ni wazoefu sana katika wizi na wanafahamu mbinu za kuiba ambazo wewe huwezi hata kuziwaza hivyo hata ikiwa utakuwepo muda wote bado wanajua namna ya kufanikisha malengo yao tena pengine kwa uhakika kuliko hata usipokuwepo. Hii ni kwa sababu wao ndio wataalamu na utakuwa unawasikiliza kwa mengi ya kitalaamu wanayokwambia hivyo ni rahisi kukupotosha wakishirikiana na watu wengine wote utakaojihusisha nao kuhakikisha mipango yao inakwenda kama walivyopanga.

Lakini pia mradi wa ujenzi unahitaji muda mwingi sana na umakini mkubwa kwenye kushughulika nacho kitu ambacho watu wengi hawawezi kwani hawana muda wote huo wa kupoteza kiasi hicho. Muda wako una thamani kubwa sana ukilinganisha na jinsi unaupoteza kwenye jambo ambalo ungeweza kulifanikisha kwa mafanikio makubwa bila kuupoteza. Hii ni hasa ukizingatia kwamba wewe sio mtaalamu hivyo uwepo wako bado hautakamilisha ubora na usahihi wa ujenzi unaolenga japo utasaidia kupunguza uharibifu. Habari njema ni kwamba kuna njia nzuri sana na za uhakika za kukuondolea usumbufu wote huo.

Sasa ili kudhibiti kuibiwa na zaidi kudhibiti kufanyiwa kazi isiyo na kiwango kwanza unapaswa kujitahidi kufanya kazi na watu wa kuaminika badala ya mafundi ambao hawana mfumo wowote wa udhibiti wala sifa wanayoijenga. Na hapa unapaswa kuchagua kampuni ambayo inafanya ujenzi kwa gharama nafuu ambazo ni karibu sawa na gharama za kawaida za mafundi mtaani lakini wenye mfumo bora wa udhibiti na inayojaribu kulinda sifa yake ili kuendelea kuaminiwa. Kampuni licha ya kulinda sifa ya uaminifu lakini pia inazingatia ubora ambao ni sehemu ya sifa inayojengwa. Baada ya kupata kampuni nzuri inayojenga kwa gharama nafuu kinachofuata baada ya hapa ni kuisainisha kampuni mkataba kwamba mwishoni mwa mradi kabla ya makabidhiano utafanyika ukaguzi wa kiataalamu utakaofanywa na mkadiriaji majenzi juu ya vifaa vilivyotumika na ikiwa kuna udanganyifu basi kampuni hiyo itawajibika kulipa upotevu huo pamoja na adhabu juu yake.

Kwa kuwa lengo lako ni kupunguza gharama kampuni hiyo utaipa mkataba wa ufundi peke yake ambapo vifaa utanunua mwenyewe ili kuhakikisha kwamba unapata pia kwa bei nafuu na hivyo kushusha gharama. Hapo sasa itabidi kuwa na watu wa pande zote mbili ambao watahakikisha wanaandika vifaa vinavyoingia kwenye eneo la ujenzi na kukibidhiana kwa maandishi pia. Hii itasaidia wakati wa ukaguzi kupunguza kazi na ugumu wa kupata taarifa sahihi.

Kwa huduma bora za ujenzi na uhakika wa ubora na uaminifu karibu kufanya kazi na kampuni yetu ambao kauli mbiu yetu kuu ni uwazi, uaminifu na uwajibikaji. Tunafanya miradi ya aina zote za majengo kila mahali Tanzania na hata nchi Jirani. Tupigie kwa namba hizi hapa chini sasa kwa maelezo na ufafanuzi zaidi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *