HIZI NDIZO SABABU ZA KWA NINI UNAPASWA KUUNGANISHA RAMANI NA UJENZI.

Kwa mazoea yaliyopo mtaani watu linalopokuja suala la kujenga huwa wanaanza kwa kutafuta mtaalamu wa kuchora ramani ambaye hufanya kazi ya kutengeneza na kukamilisha michoro ya ramani kisha huenda sasa kutafuta fundi au mafundi kwa ajili ya ujenzi wa jengo lake. Haya ni mazoea ambayo yanasababishwa na mtazamo fulani wa watu au ushauri ambao watu huchukua kwa marafiki, ndugu, jamaa au watu wengine ambao walishapitia uzoefu husika. Hata hivyo kuna manufaa mengi zaidi za mtu kujenga na watu au kampuni yenyewe iliyofanya michoro ukilinganisha na kutafuta mtu wa tofauti kwenda kufanya kazi hiyo. Manufaa hayo ni kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa nyumba inapojengwa na mtu aliyesimamia kazi ya michoro usimamizi wa kazi ya ujenzi unakuwa rahisi na unakuwa kama ni wa bure kabisa kwa sababu aliyechora ndiye anayetekeleza kile ambacho amekifanyia kazi bila kuhitaji kuzungumza na mtu mwingine au kushauriana na mtu mwigine wa tofauti. Hili linapelekea kazi ya usimamizi kuwa rahisi na isiyo na gharama kabisa au ya bure kabisa ukilinganisha na kutumia fundi ambapo utahitaji tena mchoraji aje kukagua maendeleo na kama sio hivyo ujenzi utakuwa wa viwango duni.

Ujenzi wa nyumba unapofanywa na mchoraji uhakika wa ujenzi kufanyika kwa usahihi bila kuja na makosa mengi ya kujirudia ni wa uhakika sana. Hii ni kwa sababu kile ambacho alikiona na kukidhamiria kinaenda kufanyika hivyo hivyo na hawezi kuvumilia namna yoyote tofauti. Hata inapotokea kunahitajika mabadiliko fulani katikati ya mradi wa ujenzi basi kazi huwa ni rahisi sana kwa sababu mchoraji mwenyewe ndiye ana mfumo tete uliotumika kufanya kazi ya michoro na anaona ni kitu gani kinaweza kufanyika na usahihi wake utakaohitajika kufanyika. Hili ni muhimu hata kwenye kuondoa mivutano baina ya mafundi watekelezaji na wataalamu wachoraji ambayo hutokea mara kwa mara na kuharibu kazi wakati kila mtu akijaribu kutetea maslahi yake.

Hivyo ni muhimu zaidi pale mtu unapoamua kujenga basi kutafuta mtu/watu au kampuni ambayo inafanya vyote kwa pamoja kwani hata gharama zenyewe za ujenzi kwa kampuni ndogo huwa sio kubwa sana ukilinganisha na mafundi wa mtaani. Sasa ili kufanikisha zoezi zima la ujenzi wa kuunganisha ramani na ujenzi kwa mtu/watu au kampuni hiyo hiyo tupigie sasa hivi kwa mawasiliano yafuatayo hapa chini.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *