HAKUNA ANAYEJUA GHARAMA ZA UJENZI KWA UHAKIKA, USIDANGANYIKE.

Watu wengi wanaamini kwamba kwa kuwa mtu amejihusisha na ujenzi kwa muda mrefu au kwa kuwa mtu ni mhandisi au msanifu wa ujenzi mwenye uzoefu basi anaweza tu kufahamu gharama za ujenzi wa jengo lolote atakaloonyeshwa. Kwa sababu hiyo wapo watu wengi ambapo wengine ni wataalamu kwenye sekta ya ujenzi huku wengine wakiwa ni mafundi wenye uzoefu wakijiamini na kuaminisha wateja mbalimbali kwamba ujenzi fulani utagharimu kiasi fulani cha fedha. Ukweli ni kwamba hayo mara zote huwa ni makisio tu ambayo hayana uhakika wala sio rahisi gharama iwe kamili kama wanavyokisia bali kama wako makini kwenye mahesabu ya ujenzi basi gharama inaweza kuwa katika wastani huo. Na kama wakikosa umakini kidogo sana gharama inaweza kuwa ni tofauti kabisa.

Jambo ambalo linatakiwa likushangaze zaidi ni kwamba sio tu mafundi na wahandisi ndi wanabahatisha tu kwenye gharama sahihi za ujenzi bali hata wataalamu wenyewe wa ukadiriaji majenzi maarufu kama Quantity Surveyors au QS nao bado huwa hawana usahihi wa asilimia zote kwenye makadirio yao ya gharama za ujenzi. Wanachofanya ni kuhakikisha kwamba vyote vinavyokwenda kutekelezwa vinapigiwa mahesabu sahihi lakini kwa sababu mbalimbali hesabu hizo zinaweza na kupanda au kushuka kwa sababu mbalimbali ambazo zinaweza zisionekane na mtu yeyote kwa kipindi chote.

Hivyo mahesabu ya gharama za ujenzi yatafanyika na kukaribia kupatia gharama sahihi alkini sio kwa kiasi kikubwa ambapo kuna vifaa vya aina zote. Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo zinaweza kufanyika kwa umakini zaidi japo sio makadirio ya asilimia mia moja. Karibu sana kwa huduma nyingine zote za ujenzi kwa uhakika kabisa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *