HIZI HAPA SABABU ZA KWA NINI, LAZIMA UTAJUTIA MAAMUZI YAKO KWENYE MRADI WA KWANZA WA UJENZI.

Kitu cha kwanza ambacho utakuta kujutia ambacho watu wengi pia hujutia sana baadaye wakati unafanya ujenzi kwa mara ya kwanza ni kukosa uelewa juu ya gharama za ujenzi. Mara watu hufikiri kwamba kuna namna wanaweza kupunguza gharama za ujenzi hivyo hujaribu kuvutiwa na watu wanaoonekana kumwambia kuhusu gharama kidogo kwenye ujenzi bila kujihangaisha na uhalisia kwa sababu hilo ndilo wanalotaka kusikia. Kinachotokea ni kwamba anakuja kukuta ile gharama ndogo aliyoambiwa haikuwa kweli bali wale waliomwamba walifanya hivyo ili tu kumfurahisha akubali kuanza kazi na kuwapa lakini anagundua kwamba anatakiwa kuongeza sana fedha kwenye vifaa na hata ufundi kwani vifaa vyote alivyoaminishwa kwamba vitatosha vimeisha na kazi bado sana. Kitu cha muhimu kujifunza hapa ni kwamba wakati wa kuuliza gharama watu wengi watakwambia gharama ndogo ili tu ukubali kuanza kazi na kuwapa kwa sababu wana shida na pesa lakini haitachukua muda mrefu na utapaswa kukubaliana nalo kwani hata wewe mwenyewe unajionea kwamba vifaa havijatosha. Lakini wakati mwingine utakuta ni wewe mwenyewe ulijidanganya kuhusu gharama lakini mara nyingi utakuta ni kubwa sana kuliko ulivyotegemea mwanzoni.

Jambo la pili ambalo mtu utajutia wakati unajenga kwa mara ya kwanza ni kwa nini hukuweka kipaumbele kwenye ubora zaidi kuliko ambavyo uliamini labda sio muhimu. Hii hutokea kwa sababu akili yako kwa mara ya kwanza itakuwa imekaa kwenye gharama pekee na vitu vingine vyote utakuwa unaamini bila mashaka kwamba vitakwenda vizuri tu japo huna uzoefu nao. Kimsingi kitu ambacho unahitaji zaidi kwenye jengo lako ni ubora na usahihi wa kazi kuliko kitu kingine chochote kabla, suala la gharama huja kama kipaumbele cha pili baada ya kipaumbele cha kwanza ambacho ni ubora na usahihi wa jengo kuwa umetimizwa. Lakini suala la ubora na usahihi wa jengo huweza kwenda tofauti kabisa na mategemeo kama mtu hutaliwekea kipaumbele pia, na hili hutokea ka sababu mbalimbali ambazo nyingine huwezi hata kuzitegemea. Ikitokea umeshindwa kuweka kipaumbele katika ubora na usahihi wa jengo lako halafu likafanyika kwa makosa huweza kukuingiza kwenye hasara kubwa kulirekebisha mpaka ukajutia kwamba gharama hiyo hailingani kabisa na kile ulichokuwa unajaribu kukwepa. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia pia ubora na usahihi wa jengo kama kipaumbele cha kwanza ili kudhibiti gharama hizi.

Jambo lingine la tatu ambalo huenda ukajutia kwenye ujenzi wa jengo lako ni muda utakaotumia kukamilisha ujenzi huo. Hakuna kitu kwenye ujenzi ambacho huwa kinachukuliwa kwa urahisi kama muda, yaani watu hutegemea kwamba jengo husika litakuwa limekamilika ndani ya kipindi fulani lakini katika uhalisia hilo hushindwa kutokea kwa sababu utakuta kunakosekana mpango kazi ambao umapangiliwa kwa umakini na kwa kuzingatia kila kitu ambao utaweza kufanikisha ujenzi husika kumalizika ndani ya muda. Hata hivyo mpango kazi huo huhitaji kuhakikisha kwamba pande zote zinatimiza majukumu na wajibu wao ili nao uweze kukamilika kama ulivyopangwa kitu ambacho mara nyingi kinashindwa kutokea. Hivyo ni muhimu sana mtu unapokuwa unahitaji jengo husika liwe limekamilika ndani ya kipindi fulani basi na mpango kazi ufanyike kwa umakini mkubwa ukizingatia muda uliopangwa ambao unaendana vizuri na kile kinachokwenda kufanyika.

Stress engineer or architect with laptop and tablet holding hands at his head. He is having problems in work. Engineering concept.

Jambo la nne na ambalo huwashangaza wengi kwani hufanyika na watu ambao walitegemea ni watu makini na wanaojiheshimu ni suala zima la wizi wa vifaa vya ujenzi. Wizi wa vifaa vya ujenzi ni kitu ambacho mara nyingi kinafanya na mafundi wa ujenzi ambapo ni utamaduni wao hivyo ikiwa hakutakuwa na udhibiti basi wizi ni lazima utatokea hususan kama unafanya kazi na mafundi wa mtaani. Changamoto ya wizi ni kwamba mara nyingine unaweza kuibiwa sana lakini usijue kama umeibiwa kwa sababu mafundi ni watu wenye uzoefu na akili nyingi katika kufanikisha mambo yao kwa namna ambayo wewe huwezi kujua kwa sababu kwanza ni utamaduni wao na wana njia nyingi sana za kukuhadaa. Hivyo japo utapewa watu hao na watu wa karibu unaowaamini na wao wanaamini kwamba hao ni watu wazuri na sahihi lakini bado wana nafasi kubwa ya kufanya hivyo na hata wewe kama usipojua huenda bado ukawaambia watu wengine kwamba hao ni watu bora sana japo nawe walikuibia lakini hukuweza kugundua. Mbinu zao za kuiba ni nyingi ikiwemo kushirikiana mpaka na wenye maduka ambako watakuagizia wewe kwenda kununua huko vifaa vya ujenzi.

Sasa ili kuepuka majuto yote hayo hapo juu unapaswa kufanya maamuzi sahihi ya kutafuta washauri wa kitaalamu wa kukushauri namna ya kuenenda ikiwa ni sambamba na kutumia kampuni ya watu waaminifu wenye gharama nafuu kukufanyia kazi yenye ubora na kwa uaminifu mkubwa na kuwa kuzingatia muda ulioupanga. Karibu sana kwenye timu yetu ya ujenzi makini ambayo imejikita kwenye ubora na uaminifu kukusaidia kukamilisha ujenzi wako bila kujali ni mradi mkubwa au mdogo kiasi gani. Kwa mawasiliano tupigie au kutuma ujumbe whatsapp au kawaida kwa namba za simu hapo chini ili kuepuka majuto na kuishia kuwa mwenye furaha sana na kuridhika mwishoni wa mradi wako wa ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *