KUFANYA UJENZI NA KAMPUNI AU KUFANYA UJENZI NA MAFUNDI.

Watu wengi wanajua kabisa kwamba kufanya mradi wake wa ujenzi na kampuni kuna faida nyingi na muhimu kuliko kufanya ujenzi na mafundi wa mtaani. Watu wanajua kwamba manufaa wanayoweza kupata kwenye kampuni ni pamoja na kufanyia kazi kwa uaminifu, kazi kutokukimbiwa, kusaidiwa kutatuliwa changamoto za kwenye halmashauri za miji, manispaa na majiji, mradi kupangiliwa vizuri kimahesabu na kimpangokazi, kuepuka usumbufu mwingi usio wa lazima, kupewa ushauri wenye manufaa ya muda mrefu badala ya kuangalia tu manufaa binafsi ya muda mfupi.

Lakini pamoja na yote hayo bado utakuta watu wengi wanatafuta tu mafundi wa mtaani wa kuwafanyia kazi zao zilizochorwa kwa ustadi mkubwa na kuogopa kabisa kutumia kampuni. Je sababu ni nini inayowafanya watu kuogopa kampuni? Hapa sababu kubwa ni mbili, ya kwanza ni mazoea ambayo yamekuwepo kwamba nyumba huwa inajengwa na fundi na namba mbili ambayo pengine ndio yenye nguvu zaidi ni imani kwamba kampuni zina gharama kubwa sana na mafundi wana gharama ndogo.

Sasa leo nataka nikwambie kwamba watu wengi hawajui kwamba hiyo sababu ya pili haina ukweli katika uhalisia. Hao mafundi ambao watu hufikiri wana gharama nafuu kwenye ujenzi gharama zao mara nyingi hazitofautiani sana na gharama za makampuni ya kawaida. Wastani wa gharama za ujenzi kwa mafundi na makampuni ni huo huo na wakati mwingine mafundi huwa na gharama kubwa kuzidi hata kampuni pale wanapoona wamepata kazi nyingi za kujenga. Jambo hili tumeshakutana nalo mara nyingi sana sisi kama kampuni pale tunapojikuta tunahitaji mradi fulani wa ujenzi na kukuta mafundi walioomba wamedai pesa kubwa kuliko sisi wenye kampuni.

Tofauti pekee iliyokuwepo ya kwa nini kampuni inachaji pesa sawa na mafundi wakati ina gharama nyingi za kulipa ambazo zinatakiwa zitokane na faida kubwa ambayo imetokana na gharama kubwa wanazochaji wateja wao. Kampuni inakuwa na faida kupitia wingi wa miradi inayokuwa inaiendesha tofauti na fundi ambaye hana mfumo wa ufanyaji kazi wala udhibiti na kuishia kufanya kazi moja pekee kwa hiyo anakuwa hana namna nyingine ya kupata fedha nyingine mpaka amemaliza mradi husika. Hivyo ni muhimu sana kutumia kampuni kwani usalama ni mkubwa kabisa na suala la gharama ni zile zile, na ubaya zaidi mafundi wakiwa wezi tena ambapo wengi kweli huwa ni wezi zaidi ya 95% hivyo gharama huwa zinakwenda juu zaidi na zaidi nab ado ubora na utaalamu ukakosekana pia.

Kwa kampuni inayofanya kazi zake kwa viwango bora kabisa na gharama nafuu tuwasiliane kwa mawasiliano haya hapa chini.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *