SAKAFU YA JENGO.
Unapofikiria kumalizia sakafu ya jengo ni lazima ujiulize umalizia wake wa uso wa juu kabisa unakuwaje.
-Kiwango cha utelezi; epuka kumalizia na uso wa sakafu unaoteleza sana au laini sana maeneo ya bafuni na kwenye vibarazani.
-Kiwango cha upukutikaji; epuka kumalizia na uso wa sakafu unaopukutika kiurahisi kwenye maeneo yanayotumiwa wa kukanyagwa na watu wengi. Malighafi kama mabo na mbao zinapukutika kiurahisi wakati tailizi za saruji na terazo hazipukutiki kiurahisi.
-Kiwango cha kuathiriwa na kemikali; baadhi ya malighafi zinazotumika kwenye uso wasakafu haziendani na kemikali za asidi kwa hiyo hazifai maeneo ya jikoni.
-Hali ya hewa; malighafi kama mbao na makapeti yanaonekana kuwa makavu na yasiyoshika baridi hivyo yanafaa sehemu za baridi wakati tailizi na aina za mawe zinaonekana kuwa na baridi hivyo zinafaa zaidi sehemu za joto.
Na Architect Sebastian Moshi
+255717452790
Let’s build the nation.
Sure, brother.