MADIRISHA YA UPVC

UPVC ni aina Fulani ya plastic ngumu ambayo mara nyingi huchanganywa na chuma ndani ili kutengeneza fremu za madirisha milango au aina nyingine za malighafi za ujenzi. Kutokana na muonekano bora wa PVC siku hizi imekuwa ikitumiwa sana katika ujenzi hasa kwenye maeneo ya madirisha na milango.

DIRISHA LA PVC

FAIDA ZA MADIRISHA YA UPVC

-Madirisha ya UPVC yanadumu sana ukilinganisha na mbao au aluminium, kwa sababu kwanza hayaathiriwi na wadudu kama mchwa wala joto kali.

-Madirisha ya UPVC ni mepesi kubeba na kusafirisha n ahata kutumia lakini pia hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara baada ya kuyaweka hivyo yanakuwa na unafuu kwenye gharama kwa sababu ukiweka umeweka.

-Madirisha ya UPVC ni mazuri sana katika kuzuia au kupunguza sauti kuingia ndani ya nyumba. Inashauriwa kutumiwa UPVC kwenye maeneo yenye kelele kama vile maeneo ya karibu na viwanja vya ndege, kanisa, msikiti, karibu na barabara kuu za magari n.k.,.

-Madirisha ya UPVC yanasaida pia kuzuia joto au baridi kuingia ndani ya nyumba hivyo joto la ndani linakuwa katika kiwango sahihi muda mwingi n ahata kupunguza gharama za kulazimika kutumia vifaa au mashine mbalimbali zinatumia umeme kuongeza ua kupunguza joto hivyo inapunguza gharama.

DIRISHA LA UPVC DOUBLE GLASS

CHANGAMOTO ZA MADIRISHA YA UPVC

-Madirisha ya UPVC ni ya gharama kubwa sana ukilinganisha na madirisha ya kawaida ya mbao au aluminium. Gharama ya madirisha ya UPVC yanaweza kufikia hata mpaka mara tatu ya gharama ya madirisha ya kawaida ya aluminium.

-Upatikanaji wa UPVC sokoni uko chini zaidi ukilinganisha na mbao na aluminium hivyo wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kupata kiasi unachotaka kwa muda unaotaka.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *