NAMNA YA KUZUIA MAJI KUVUJA VYOONI NA BAFUNI

Kuna njia kadhaa za kuzuia maji yanayoweza kuvuja vyooni na bafuni lakini hapa tutazungumzia njia kubwa mbili.

  1. Kutengeneza “suspending ceiling” yenye urefu wa kama futi moja kuteremeka chini kutoka kwenye sakafu(slab) ya juu ambapo itatengeneza eneo ambalo litawekwa matenki ya maji ya chooni na bafuni kisha kufungiwa vizuri na zege ambali limechanganywa kemikali au karatasi ya kuzuia maji kuvuja. Vifaa vyote vya mabomba ya maji vinafungiwa kabisa kwa ndani na haiwezekani kabisa kuvufikia tena.
Mifumo ya maji taka ndani ya “Suspended Slab”
  1. Aina ya pili ni inatengenezwa “suspending ceiling” au “false ceiling” chini ya slab ya chooni au bafuni iliyopo ambayo itakuwa na uwazi upande mmoja ambapo vifaa vyote na matenki ya maji ya chooni na bafuni yanawekwa hapo lakini upande huu utakuwa wazi kiasi kwamba mtu ataweza kuingia hapo na kufanya marekebisho ikiwa kuna hitilafu. Njia hii inasaidia kwamba ikitokea maji yanavuja unaweza kufanyika ukarabati bila ugumu au hata mfumo mzima wa maji ya chooni na bafuni kubadilishwa.

-Njia nyingine inayoweza kutumika ni kwa kutumia zulia la plastiki kwa kuta zote na sakafu ya chooni na bafuni au angalau kwa sakafu ya chini peke yake.

Mifumo ya maji taka kwenye “drop slab”

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *