MALIGHAFI VIOO

Kioo imekuwa ni malighafi inayomvutia sana binadamu tangu ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya ujenzi miaka zaidi ya 2500 iliyopita, wakati huu ikihusishwa kuwa na uwezo wa ziada na nguvu za kimiujiza. Kioo ni kati ya malighafi za ujenzi za zamani sana wakati huo ikiwa bidhaa hadimu na ghali sana vikiwekwa kwenye nyumba za watu mashuhuri pekee kama wanasiasa wa himaya ya Rumi ya kale.

Vioo vilianza kutumika kwenye makanisa kuanzia miaka ya 600 baada ya Kristo

-Vioo vya mwanzo kabisa vya asili vilivyopatikana katika maeneo ya volcano maelfu ya miaka iliyopita na vingine vilivyoptokea kwa asili baada ya radi kupiga kwenye mchanga vilitumika kutengeneza silaha. Wakati vioo vilivyotengenezwa na binadamu vilitumika kwa ajili ya urembo, mapambo, kwenye meli za usafiri na hata kutengenezea vyombo vya nyumbani kama sahani.

Kukua kwa teknolojia ya vioo

-Teknolojia ya kutengeneza vioo kwa kutumia upepo maarufu kama “glass blowing technogy” iliyogunduliwa katika karne ya kwanza huko Ulaya ilileta mapinduzi makubwa katika fani ya kutengeneza vioo. Mbinu hii ilisambaa sana wakati wa himaya ya Rumi ya kale. Uzalishaji wa vioo vyenye uwazi(clear glass) kwa kutumia “manganese dioxide” ulipelekea vioo kuanza kutumika katika majengo mbalimbali na madirisha ya vioo yakaongezeka sana na kuongeza ushawishi kwenye majengo wakati wa himaya ya Rumi ya kale. Miaka mingi baadaye vioo viliendelea kutumika zaidi katika majengo mbalimbali Ulaya na mashariki ya kati na baadaye katika karne ya 7 vioo vilianza kutumika sana katika makanisa na taasisi nyingine za dini.

Teknolojia ya vioo iliendelea kuimarika na kurahishwa kiasi cha kutumika kwa kiasi kikubwa zaidi.

-Hata hivyo vioo viliendelea kuwa ni malighafi ya gharama kubwa na inayotumiwa na watu wachache mashuhuri na matajiri inayozalishwa kwa gharama kubwa kwa kutumia nguvu na akili nyingi. Baada ya mwaka 1958 mapinduzi makubwa kwenye teknolojia ya utengenezaji vioo yaliyoletwa na Pilkington yalirahisisha utenezaji vioo na kupelekea kukuza sana matumizi yake kwenye ujenzi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *