USIAMINI KIURAHISI, MWAMBIE AKUONYESHE KAZI ALIZOFANYA

Unapohitaji mtu sahihi wa kukufanyia kazi kwa viwango makini unachohitaji sio watu wa kupendekezwa peke yake bali unahitaji kuona kazi iliyofanywa na mtu husika kwani hiyo ndio kipimo sahihi cha uwezo wake.

KAZI ALIYOFANYA NDIO KIPIMO SAHIHI CHA UWEZO WAKE

1. Watu wengine wanaweza kujieleza vizuri zaidi ya wanavyoweza kufanya kazi na kuna watu wana ushawishi mkubwa sana wa maneno lakini kwenye vitendo hawana viwango wala nidhamu ya kazi.

KUJIELEZA VIZURI SIO KIGEZO PEKEE CHA KUAMINI UBORA MTU KAMA BADO HAJAONYESHA VIWANGO VYAKE VYA KAZI

2. Kufanya kazi zenye ubora wa viwango vya juu ni tabia. Watu huwa wanafikiri kufanya kazi ya viwango vya na nidhamu katika kazi vinasababishwa na uwezo peke yake, hili sio kweli ndio maana unaweza kukuta mtu anafanya kazi nzuri sana chini ya usimamizi na ana uwezo mzuri akisimamiwa na kutakiwa kufanya kazi ya viwango fulani lakini anapofanya peke yake kwa sababu kazi yenye ubora sio tabia yake wala sio kitu anachojali sana na hapo ndipo utakaposhangaa atakavyofanya kazi ya hovyo. Hivyo inalazimu kwamba ikiwa unahitaji mtu wa uhakika mwenye uwezo utalazimika kumtaka akuonyeshe kazi alizofanya chini ya usimamizi wake mwenyewe.

KUFANYA KAZI ZA VIWANGO VYA JUU NI TABIA SIO UWEZO PEKE YAKE

3. Wakati mwingine unaweza kupewa pendekezo la mtu fulani kwamba anafaa, kumbe aliyempendekeza naye anamsikia lakini uhalisia wa mtu huyo hana uwezo wa kutosha kukidhi viwango sahihi vya ubora unavyovitazamia hivyo unapaswa kwanza kumtaka akuonyeshe amefanya nini na kwa viwango gani kabla hujaamua kumwamini kwa kazi unayotaka kumpa.

USIOGOPE KUHAKIKI UWEZO WA MTU ULIYEPENDEKEZWA KUEPUKA MAJUTO YA BAADAYE

Usiogope wala kusita kutaka mtu akuonyeshe kazi alizosimamia mwenyewe ili uweze kujua kwa uhakika uwezo wako halisi kwani ikiharibika na ukaingia hasara utajilaumu, utajutia na utamchukia sana pia. Kuhitaji kuona kazi alizofanya ni sehemu ya wewe kupigania ubora wa kazi yako unayoithamini na unayokwenda kuweka pesa zako nyingi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *