FANYA UKAGUZI WA JENGO LAKO MARA KWA MARA.

Kufanya ukaguzi wa jengo au nyumba yako mara kwa mara ni jambo muhimu lakini wengi wamekuwa hawazingatii na hivyo wanakuja kujikuta wanalazimika kujenga ukuta kwa uzembe wa kushindwa kuziba ufa. Inapaswa kuwa na kipindi maalum cha kufanya ukaguzi wa jengo hata kama unaliona lipo katika hali nzuri kwa nje, inaweza kuwa ni kila baada ya kipindi cha mwaka mmoja au kila baada ya mvua za masika n.k., na hili litakuwa na manufaa makubwa kwako.

UKAGUZI WA JENGO UNAWEZA KUWA NI KIPINDI CHA KILA BAADA YA MWAKA MMOJA AU KILA BAADA YA MASIKA N.K.,

-Kwanza kufanya ukaguzi wa jengo lako mara kwa mara kutakusaidia kutatua tatizo kabla halijakuwa kubwa na kuhitaji nguvu kubwa na usumbufu mwingi kulitatua au pengine kabla halijashindikana kabisa kutatulika pale linapokuwa ni tatizo kubwa sana tayari.

UKAGUZI WA MARA KWA MARA UNASAIDIA KULIFAHAMU TATIZO KABLA YA KUWA KUBWA NA KUWA CHANGAMOTO KUBWA

-Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa jengo lako kutasaidia kupunguza gharama za kulitatua tatizo/changamoto kwa sababu utaweza kuifahamu mapema kabla haijawa kubwa kiasi cha kuhusisha gharama kubwa sana kuitatua au kabla haijaleta madhara makubwa sana pia.

UKAGUZI WA MARA KWA MARA UTAPUNGUZA GHARAMA ZA UKARABATI WA JENGO

-Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa jengo lako kutasaidia kuepusha hatari za ghafla ambazo hujitokeza na kusababisha maafa makubwa, kwa mfano nyumba kuungua kutokana na tatizo la shoti ya umeme ambayo imejitokeza lakini haikuweza kujulikana haraka na hivyo kusababisha hasara kubwa ya uharibifu wa mali au hata watu kupoteza uhai kwa sababu hata mifumo ya kisasa ya kuzima moto majengo mengi hayana, au kesi za majengo kuanguka na kusababisha vifo na uharibifu wa mali. Lakini pia inaweza kuwa ni mfumo wa maji kuziba na kuanza kuozesha baadhi ya maeneo hasa yale yenye chuma zinapiga kutu na kuanza kuoza, yote haya yanaweza kuzuia na ukaguzi wa mara kwa mara.

UKAGUZI WA MARA KWA MARA UTAEPUSHA HATARI NYINGI KAMA VILE AJALI YA MOTO AU JENGO KUANGUKA

-Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kunasaidia kwenye kuhakikisha jengo liko katika muonekano mzuri na unaovutia muda wote kwani ukaguzi unagundua mapungufu yanayopelekea muonekano kufifia, hivyo kupendekeza maboresho.

UKAGUZI WA MARA KWA MARA UTALIWEKA JENGO KATIKA MUONEKANO BORA WAKATI WOTE

NOTE: Thamani ya jengo huendelea kupungua kwa kadiri muda unavyokwenda lakini kuna maeneo ya kwenye jengo hasa yenye udhaifu ambayo hayakufanyika kwa usahihi unaotakiwa ambapo hupoteza ubora wake kwa haraka zaidi lakini bila kujulikana mapema na kuleta uharibifu mkubwa, maeneo haya pamoja na mengine yanaweza kufahamika kupitia ukaguzi wa jengo wa mara kwa mara ambao utapelekea maboresho yatakayoepusha hasara kubwa ya tatizo kuwa kubwa.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *