AINA ZA KUCHORA NA KUJENGA/DESIGN AND BUILD TYPES

  1. Timu ya mradi inapoongozwa na mkandarasi(Contractor Led Design + Build)

Katika njia ya kufanikisha mradi wa ujenzi ya kuchora na kujenga(design and build) kwa aina ya timu ya ujenzi kuongozwa na mkandarasi ambaye ataajiri na kuingia mkataba na wataalamu wengine wa ujenzi pamoja na watoa huduma wengine kwenye kufanikisha mradi huu uzito mkubwa mara huwekwa kwenye bajeti iliyopo. Kwenye aina hii ya kuchora na kujengwa kwa kuongozwa na mkandarasi gharama za mradi zinakuwa kipaumbele cha kwanza kabla ya maono, malengo, ubora, aina na muonekano wajengo n.k.,

TIMU YA MRADI IKIONGOZWA NA MKANDARASI KIPAUMBELE CHA KWANZA NI GHARAMA

2. Timu ya mradi inapoongozwa na msanifu majengo(Architect Led Design + Build)

Njia nyingine ya kuchora na kujenga ni ile ambayo timu inayoenda kufanikisha mradi husika inapoongozw ana msanifu majengo anayebuni na kuchora jengo lenyewe. Katika aina hii ya kufanikisha mradi uzito mkubwa ua kipaumbele cha kwanza huwa aina na staili ya jengo pamoja na ubora wa kibunifu wa jengo lenyewe, kisha kipaumbele namba mbili huwa ni mahitaji ya mteja na kipaumbele namba tatu ndio huja gharama za mradi wenyewe.

TIMU YA MRADI IKIONGOZWA NA MSANIFU MAJENGO KIPAUMBELE HUWA NI UBORA WA KIBUNIFU WA JENGO

3. Timu ya ujenzi inapoongozwa na maslahi ya mradi(Project Led Design + Build)

Katika aina hii ya kuchora na kujenga(design and build) mradi na maslahi ya mradi huwa ndio kipaumbele namba moja kabla ya mambo mengine yote na hapa mteja huwa anasikilizwa zaidi juu ya ni nini anakilenga kwenye mradi husika na hicho ndicho kinakuwa kinaamua vitu vingi zaidi juu ya mradi husika kutegemea na malengo yake.

TIMU YA UJENZI INAPOONGOZWA NA MALENGO YA MASLAHI YA MRADI CHA KWANZA HUWA NI MALENGO YA MRADI

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *