MAMBO MUHIMU AMBAYO MTEJA ANATAKIWA KUJADILI NA MTAALAMU WA UJENZI KUHUSU MRADI
Kuna mambo muhimu ambayo mteja na mtaalamu wa ujenzi wanapaswa kuyajadili ili kufikia maamuzi sahihi kabla ya hatua ya kwanza ya mradi wa ujenzi, kama ifuatavyo.
Mahitaji ya mteja: Mteja anapaswa kufahamu anahitaji kuwa na vitu gani ndani ya jengo lake kwa maana ya idadi ya vyumba na nafasi nyingine katika jengo pamoja na mahitaji mengine ya ziada, hili litampa mtaalamu wa ujenzi nafasi ya kutoa ushauri sahihi.
Taarifa za kiwanja: Mteja anapaswa kutoa taarifa za kiwanja(site) cha ujenzi kama vile ukubwa wake kwa maana ya mita za mraba, urefu na upana, hali ya viwanja vya jirani na vitu vingine vinavyokizunguka kiwanja, hali ya kiwanja chenye kama ni mwinuko au tambarare, mahali kilipo kwa maana ya mji husika, hadhi yake kwa maana ya kama kimepimwa au bado. Taarifa za kiwanja zitamsaidia mtaalamu kutoa maamuzi sahihi juu ya mradi unaokwenda kufanyika.
-Vipaumbele vya mteja: Mteja anapaswa kusema vipaumbele vyake kwa mradi husika kwa maana ya nini anajali zaidi kwenye huo mradi wake na nini anategemea zaidi kukiona kikifanyika, hili litasaidia mtaalamu wa ujenzi kufahamu nini cha kukipa uzito na nini cha kukipa uzito zaidi.
-Lengo la mradi: Mteja anapaswa kusema nini lengo kuu la mradi wake huo kwa maana ya kwamba jengo hilo ni kwa matumizi gani na ya kiwango gani, kwa mfano labda ni jengo la hoteli lakini ni hoteli ya nyota tano, hilo litasaidia mtaalamu wa ujenzi kujua ni thamani kiasi gani jengo hilo linatakiwa kupewa na hata hadhi ya wanaoitumia watahitaji ukubwa wa nafasi kiasi gani.
-Maoni ya mteja: Mteja anapaswa kusema yeye binafsi ana maoni gani juu ya mradi huu ili kumsaidia mtaalamu wa ujenzi kujua fikra za mteja juu ya mradi wake ni kumsaidia kupata mtazamo sahihi kwa mradi husika.
-Bajeti ya mradi: Mteja anapaswa kumwambia mtaalamu wa ujenzi amejiandaa kiasi gani kifedha ambayo nataka kuiwekeza kwenye mradi husika ili kuweza kumshauri kwa usahihi kadiri anavyoona itaendana na bajeti yake.
Muda wa kuanza mradi: Mteja anapaswa kumwambia mtaalamu wa ujenzi ni wakati gani amejiandaa kuanza mradi husika ili kwa kuzingatia taratibu mbalimbali aweze kumshauri juu ya muda sahihi wa kufanya kila jambo na kwamba kila hatua ya mradi inaweza kuchukua muda mrefu kiasi gani.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!