UKUBWA WA NYUMBA UNATOKANA NA UKUBWA WA VYUMBA NDANI YA NYUMBA

Imekuwa kawaida kukutana na mteja anakwambia nahitaji nyumba iwe na vyumba vikubwa ndani vyenye ukubwa wa kutosha, anakwambia “nataka sebule kubwa na master bedroom kubwa” lakini mwisho anaishia kukwambia lakini nyumba yenyewe isiwe kubwa, kwa sababu anataka nyumba ambayo haitamgharimu sana fedha nyingi kuijenga.

VYUMBA VINGI NA VIKUBWA VINASABABISHA NYUMBA KUWA KUBWA

Kwanza kabisa nakubali kwamba kadiri nyumba inavyokuwa kubwa ndivyo kadiri gharama ya kuijenga inavyokuwa kubwa zaidi lakini kitu muhimu cha kufahamu ni kwamba ukubwa wa nyumba unasababishwa na ukubwa wa vyumba ndani ya nyumba.

Pale unaposema unahitaji vyumba vikubwa tena viwe vinne au zaidi tayari hapo unaongelea nyumba kubwa na sio ndogo kama unavyotamani iwe, hivyo kama unataka nyumba iwe ndogo ili ikupe unafuu kwenye kuijenga unapaswa pia kuzingatia kwamba vyumba ndani navyo viwe vidogo. Hata hivyo unaweza kuamua chumba kimoja kiwe kikubwa ambapo kitaongeza pia kidogo ukubwa wa nyumba.

KWA VIWANGO VYA MAISHA YA WATU WA KAWAIDA NYUMBA IKISHAFIKIA KUWA NA VYUMBA VINNE VYA KULALA TAYARI IMESHAANZA KUWA NYUMBA KUBWA

Lakini mwisho wa siku ni vyema kujitahidi kujenga kile hasa unachotamani badala ya kuogopa sana vikwazo vya bajeti ya fedha kwani hakuna nyumba unayoweza kuijenga kwa beo rahisi kama wengi wanavyofikiri kila nyumba ya kutosha familia kuishi huwa inakuwa na gharama. Jambo la muhimu na kuamini kwamba utaikamilisha na kuweka bidii kuikamilisha, na kwa sababu umefanya hasa kile unachopenda basi hilo litakusaidia kukupa motisha na shauku ya kujituma zaidi kuweza kufanikisha.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *