GHARAMA ZA UJENZI ZINAJUMUISHA MICHORO YA RAMANI

Watu wengi wanapofikiria kuhusu gharama za ujenzi huanza kufikiria wakati wa kujenga, yaani kuanzia kwenye kuchimba msingi huku gharama za michoro ya ramani wakizitenganisha na ujenzi wenyewe.

Jambo hili limekuwa na madhara kadhaa na limekuwa likiwaumiza wataalamu wa ujenzi na likimuumiza hata na mteja mwenyewe pia kwa sababu huwa na madhara yafuatayo.

Kwa taratibu zilizowekwa na mamlaka zinazohusika na ujenzi ni kwamba gharama za kitaalamu ni sehemu ya ujenzi na zinachukua zaidi ya 10% ya gharama zote za ujenzi kuanzia michoro mpaka usimamizi kwa sababu ya umuhimu mkubwa na thamani kubwa ambayo utaalamu huu unaongeza kwenye mradi, gharama za michoro ya ramani zinapotenganishwa na gharama za ujenzi uwiano unakosekana kati ya ubora na ukubwa wa mradi ukulinganisha na viwango vya huduma za kitaalamu zenyewe.

MAMLAKA ZINAZOHUSIKA NA UJENZI ZIMEWEKA VIWANGO VYA GHARAMA ZINAZOPASWA KWA HUDUMA ZA KITAALAMU, HIYO INAWEZA KUWA SEHEMU NZURI YA KUANZIA KATIKA KUPATANA GHARAMA SAHIHI ZA MRADI

Gharama za michoro ya ramani zinapotenganishwa na kushindwa kuwiana na gharama za ujenzi zinapelekea kazi ambayo ni ya thamani kubwa na ingestahili kufanyika kwa viwango vya juu kwa sababu gharama za malighafi na ufundi ni kubwa sana, inafanyika kwa viwango vya chini kwa sababu gharama za michoro ya ramani zimekuwa hazichukuliwi katika ule umakini ambao unalingana na mradi wenyewe.

MARA NYINGI GHARAMA ZA MICHORO YA RAMANI ZIMEKUWA HAZICHUKULIWI KATIKA ULE UMAKINI UNAOWIANA NA GHARAMA ZA UJENZI WENYEWE

Gharama za michoro ya ramani zinapotenganishwa na gharama za ujenzi zinapelekea ubora wa kazi kushuka kwa sababu ya uholela wa ufanyaji pale ambapo gharama ya kitu kama “plastering” ya jengo kuwa hata mara nne zaidi ya gharama za michoro ya ramani ambayo ndio mwongozo mzima wa kitaalamu na kimatumizi wa jengo husika.

GHARAMA ZA MICHORO YA RAMANI ZINAPOTENGANISHWA KIUWIANO NA GHARAMA ZA UJENZI HUWEZA KUPELEKEA MRADI MZIMA KUKOSA UBORA UNAOSTAHILI

Japo ni bahati mbaya sana kwamba hatua ya michoro ya ramani huja mwanzoni wakati bado mteja hajaanza kuweka pesa nyingi katika mradi hivyo kubana sana matumizi lakini ni muhimu na busara sana katika kupatana gharama za michoro ya ramani mbali na kusisitiza ubora na uzuri wa “design”, gharama za michoro ya ramani pia zizingatie uwiano wa gharama za ujenzi kwa mfano gharama za michoro ya ramani kutokuwa chini ya angalau asilimia 1.5% ya gharama za ujenzi wote. Kwa asili hii huchangia sana kwenye ubora na uzuri wa jengo husika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *