FALSAFA YA UJENZI YA “LEAN CONSTRUCTION”.

Falsafa ya ujenzi ya “lean construction” ni aina ya usimamizi wa ujenzi ambao unalenga kupunguza yale mabaki ya malighafi ya ujenzi au mabaki ya vifaa vinavyotumika kufanya ujenzi katika tasnia ya ujenzi huku ukiongeza thamani kubwa kwa wateja.

Falsafa hii ya ujenzi ya “lean construction” ambayo imeendelea kupata umaarufu mkubwa katika fani ya ujenzi duniani chimbuko lake ni kutoka katika kampuni ya magari ya Toyota nchini Japan ambapo miaka ya 1920’s ambapo iliingizwa kwenye utekelezaji katika viwanda mbalimbali vya kampuni ya Toyota nchini Japan baada ya vita ya pili ya dunia. Mfumo huu ulilenga kuongeza thamani kwa kubwa kwa bidhaa na mchakato mzima wa kumridhisha mteja huku ikipunguza mabaki na uchafu wa malighafi za ujenzi na pia kusaidia wafanyakazi kufanya kazi kwa uweledi zaidi na kufanya kazi kwa namna ambayo ina maana zaidi kwao.

Mbinu hizi za Toyota zilileta matokeo bora sana katika kampuni ya Toyota kiasi cha kupelekea kuboreshwa na kutumika nje ya fani ya utengenezaji vitu(manufacturing).

Jina hili “lean construction” lilianzia kwenye kampuni ya “Internationa Group For Lean Construction(IDLC)” ilipoanzishwa mwaka 1993. Falsafa hii ilitumika katika hatua zote za ujenzi kuanzia kwenye uandaaji wa michoro mpaka mradi kukamilika na sio tu katika kujenga peke yake.

Mwaka 1997 Glenn Ballard na Greg Howell wa nchini Marekani waliamua kuanzisha taasisi ya “Lean Construction Institute” katika juhudi za kuendeleza na kushirikisha taarifa za kuboresha mbinu mbalimbali za usimamizi wa ujenzi

Tutaendelea kuangalia misingi ya falsafa hii ya ujenzi ya “lean construction” katika makala zinazofuata.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *