JENGO LINATAKIWA KUWA NA UWIANO NA MTIRIRIKO SAHIHI
Tunapozungumzia kuhusu jengo tunazungumzia kuhusu mpangilio wa vipengele vyote vinavyounda jengo husika bila kujali kama vimepangiliwa kwa usahihi au kimakosa. Tunapozungumzia uzuri wa jengo tunazungumzia mpangilio sahihi wa vipangele vyote vya kisanifu vinavyounda jengo husika.
Sasa jengo lolote lililofanyika katika viwango na lenye ubora, mvuto na lenye muonekano unaoleta maana ni lazima liwe katika uwiano na mtiririko sahihi. Uwiano(balance) ni ile hali ya jengo kuwa na upacha, utatu na kuendelea katika mpangilio wa kipengele chochote kinachokuwepo juu, chini, kulia au kushoto wa kila kipengele. Mtiririko ni uwepo wa kipengele au vipengele ambavyo vimepangilia katika viwango vya juu sana vya usanifu ambavyo vinaleta ladha nzuri ya kuvutia sambamba na maana fulani ambayo inaongeza umuhimu fulani na kuleta lugha ya jengo inayoongea.
Hivyo jengo lenye uwiano na mtiririko sahihi ni jengo lililokamilika kwenye kila idara na linalojumuisha vipengele ambavyo vyote vina maana na umuhimu fulani na kuondoa kabisa vipengele visivyo na maana wala umuhimu wowote katika jengo pamoja na muonekano wa jengo.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!